Na Dotto Kwilasa,Dodoma.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na teknolojia ya Habari,imeridhia
kuiongezea muda wa miezi sita Kamati ya Tathmini ya hali ya uchumi kwa
Vyombo vya Habari na Wanahabari nchini ili iweze kufanya kazi yake kwa
ufanisi zaidi.
Waziri wa
Habari,Mawasiliano na teknolojia ya Habari,Nape Nauye ametoa kauli hiyo
leo Mei 23,2023 Jijini Dodoma mara baada ya Kukutana na Kamati hiyo huku
ikiomba kuongezewa muda huo kutokana na kazi waliyopewa kuhitaji
utafiti wa kina na waki taalam na muda wa miezi mitatu ambao walipewa
awali kutotosha.
Katika
hatua nyingine Waziri Nape ametoa wito kwa wadaiwa wote ambao
wanadaiwa na Vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini kulipa madeni
hayo.
Amesema tathimini
ya hali ya uchumi wa vyombo vya habari nchini inatarajiwa kutolewa mwezi
Novemba mwaka huu, huku serikali ikiwata waandishi wa habari pamoja na
wadau wa tasnia hiyo kutoa ushirikiano kwa kamati husika ili kunuru
vyombo vya habari nchini.
“Nimekutaka
na Kamati hii awali tulikuwa tumeipa miezi mitatu lakini kutokana na
umuhimu wa tasnia hii na maagizo ya Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu
Hassan ameagiza kuwa jambo hili lisifanywe kwa kuhalakishwa bali
lifanywe kwa umakini wa hali ya juu ili kuleta mabadiliko katika tasnia
hii”amesema Nape
Waziri
huyo, amesema kamati hiyo badala ya kuharakisha jambo hilo inapaswa
kufanya tafiti za kina kwa kuhusisha wadau wengi ili kupata maoni ambayo
yatakuwa na manufaa na vyombo vya habari nchini.
“Jambo
hili linasubiriwa sana na dunia watu wanataka kuona nini Tanzania
inakwenda kufanya katika kuleta mageuzi kwenye tasnia hii ya vyombo vya
habari nchini hivyo lazima tuje na kitu kinacholeta mabadilko kwa vyombo
vyetu vya habari nchini”amesema
Amesema
hadi sasa anaridhishwa na kazi ambayo inaendelea kufanywa na kamati
hiyo kutokana na kushirikisha wataalam kutoka nyanja mbalimbali ambao
wameongeza tija katika tathimini hiyo.
“Kutokana
na ramani ambayo kamati hii imeichora hadi sasa inaonyesha ni kwa jinsi
gani inakwenda kuleta mambo ambayo yatakwenda kujibu changamoto
mbalimbali zinazo ikabili sekta hii ya habari.
“Hivyo
basi nitowe wito kwa waandishi wa habari na wadau wengine wa habari
nchini kutoa ushirikiano kwa kamati hii ili ifanikishe jambo hili na
kuleta mabadiliko kwenye vyombo vya habari ambavyo vingi hivi sasa vipo
hoi”amesema Nape
Katika
nyingine waziri hiyo wa Habari amesema wakati jambo hilo likiendele
mchakato wa sheria ya vyombo vya habari pamoja na sera utaendelea na
kama itaoneka ipo haja kufanyiwa maboresho yatafanywa.
Awali
Mwenyekiti wa Kamati ya kutathmini hali ya uchumi kwa Vyombo vya
Habarai na wanahabari,Tido Mhando ameomba Serikali kuwaongezea muda
kutokana na kazi hiyo kuhitaji utafiti wa kitaalam zaidi.
Amesema kuwa yeye pamoja na wajumbe wote wamelivalia njuga suala hilo ili kusaidia vyombo vya habari na wanahabari nchini.
Kadhalika,
Mhando amesema watahakikisha jambo hilo linakamilika ifikapo mwezi
Novemba mwaka huu kwa mujibu wa muongozo waliopewa ili kulisaidia taifa.
“Matatizo
ya vyombo vya habari yapo sehemu nyingi duniani inasikitisha sana kuona
wanahabari nchini kuendelea kuwa ombaomba na kutegemea bahasha ili
waishi na kutokuwa na uhakika wa kesho yao”alisisitiza Mhando.
Kamati
hiyo iliundwa rasmi Januari 23 Mwaka huu ikiwa na Wajumbe tisa
ikiongozwa na Mwenyekiti wake Tido Mhando na Katibu ni Gerson Msigwa
ambayo inatarajiwa kukamilisha kazi yake mnamo Mwezi Novemba Mwaka
huu.
Social Plugin