Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development (TMFD) limekutana na wadau wa kimaendeleo na kufanya majadiliano mafupi ya namna ya kutumia vyombo vya habari kwenye kuhamasisha uvuvi endelevu Nchini.
Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko amekutana na wadau hao Jijini Dar es salaam na kuitambulisha TMF na kazi zake kwenye eneo la uvuvi na vyombo vya habari.
Soko amekutana na Naibu Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bwana Kjetil Schie na kujadili fursa za kutumia vyombo vya habari kwenye kuhamasisha uvuvi endelevu.
Bwana Schie amesema kuwa anafurahishwa sana na uwepo wa TMFD kwenye eneo la uvuvi kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuhamasisha uvuvi endelevu kwa kutumia vyombo vya habari
Pia mkurugenzi wa TMF mekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa shirika la maendeleo la kimataifa la JICA Bibi Murao Akari juu ya umuhimu wa kuendeleza uvuvi kwa kutumia njia bora.
Bwana Soko amesema kuwa kwa sasa TMFD inajikita kwenye kupanua uwigo wa wadau ili kufanya kazi kwa pamoja kwa nia ya kuendeleza uvuvi endelevu Nchini.
Social Plugin