Dar es Salaam.
Akiongea na wadau wa semina hiyo katika ufunguzi Kamishna Kodi za Ndani Bw. Herbert Kabyemela amewakumbusha wamiliki na watumiaji wa meghala ya kuhifadhia bidhaa ( Storage Facilities ) kusajili maghala yao kwa Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwa ni kulingana na sheria ya usimamizi wa kodi.
Kwa upande wake mwezeshaji wa semina hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi Bw Stephen Kauzeni ameelezea kiundani sheria ya fedha ya mwaka 2022 kifungu cha 45A chini ya Sheria ya usimamizi wa Kodi Sura ya 438 kinawataka wamiliki (au watumiaji) wa maeneo ya juhifadhia bidhaa, kusajili maeneo hayo kwa Kamishna Mkuu. Kifungu hicho kilianza kutumika rasmi kuanzia tarehe 1 Julai, 2022.
Na kwa upande wao wafanyabiashara wameishukuru na kuipongeza TRA juu ya semina hiyo kwani baadhi walikuwa hawana uelewa juu ya mabadililiko hayo ya sheria na kushindwa kutimiza wajibu wao wa kusajili maeneo yao ya kuhifadhia bidhaa kwa wakati.
TRA kupitia idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi imekuwa ikiendesha semina mbalimbali juu ya masuala mbali mbali ya kikodi ili kuwajengea uelewa walipakodi.
Semina hiyo imefanyika leo tarehe 10-05-2023 ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga Dar es Salaam.
Social Plugin