WAKAZI 644 WAKO TAYARI KUINGI MKATABA MAGOMENI KOTA

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 8, 2023 katika Ofisi za TBA Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu utaratibu wa manunuzi wa nyumba Magomeni Kota.

******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Gharama za ununuzi wa nyumba za Magomeni Kota umewafikia wakazi 644 na waliotayari kuingia mkataba wa makazi ambapo Wakala wa Majengo (TBA) ipo tayari kuwatambua na kutekeleza utaratibu wote wa manunuzi.

Ameyasema hayo leo Mei 8,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa kuhusu manunuzi wa nyumba hizo.

Amesema nyumba ya chumba kimoja inauzwa kwa gharama ya shilingi milioni 48,522,913 na muda wa malipo utakuwa ni wa miaka 30 huku nyumba ya vyumba viwili ikiuzwa kwa shilingi milioni 56,894,455 na muda wa malipo ukiwa miaka 30.

"Baada ya kuwajulisha wakazi 644 wa Magomeni Kota kwa barua kupitia umoja wao ambao tumekuwa tukishirikiana kwa ukaribu tunategemea ndani ya siku 14 waoneshe interest na TBA tutajibu kwa kadri watakavyotuandikia na tupo tayari kuwatambua na kutekeleza utaratibu wa ulipaji na kuingia mkataba wa mkazi mnunuzi." Amesema

Aidha ameeleza kuwa nyumba za watumishi Magomeni Kota zilizozinduliwa hivi karibuni zitaanza kutumika Juni, Mosi mwaka huu kwa gharama kwa kodi ya shilingi 870,000 kwa mwezi bila gharama jumuishi (Service Charge,) ambayo ni shilingi laki moja na elfu 30.

Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi Magomeni Kota umetekelezwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) kwa Fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama ya shilingi 50,586,997,000.00, na kabla ya Rais Samia kutoa maelekezo ya kupunguza gharama za uuzaji nyumba hizo zilikuwa zikiuzwa kwa Sh. 74 milioni kwa chumba na sebule na Sh. 86 milioni kwa vyumba viwili na sebule.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 8, 2023 katika Ofisi za TBA Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu utaratibu wa manunuzi wa nyumba Magomeni Kota.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 8, 2023 katika Ofisi za TBA Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu utaratibu wa manunuzi wa nyumba Magomeni Kota.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post