WANAWAKE WANAOTOKA FAMILIA ZA KICHUNGAJI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KIUCHUMI


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joab Ndugai.

Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Anglikana Tanzania (UMAKI) Margareth Ndonde amewataka wanawake wa familia za kichungaji kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo kujihusisha  ili kuepuka kuwa tegemezi na  kuwatwisha  mzigo waamini.

Amesema hayo kwenye Uzindizi wa mradi wa maendeleo ya Kanisa na Jamii uliyofanyika Chuo cha Theolojia cha Mt Philip's Kongwa mkoani Dodoma unaotekelezwa katika vijiji kumi kwa ukanda wa Hogoro na Zoissa.

Katibu huyo amesema ikiwa Wanawake hao watakubali kujibidiisha wataongeza ustawi kwenye  familia zao na kuwa bora zenye kujitegemea na kuwa mfano kwa wengine.

"Kwenye familia zetu imezoeleka tunapenda kuwa tegemezi,ni wakati wetu Sasa kuukataa umaskini Kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na  kujenga mahusiano mema na majirani ili kuimarisha amani na upendo katika jamii,"amesisitiza.

Naye Spika wa bunge aliyemaliza muda wake Job Ndugai ametumia nafasi kuitaka jamii kuwekeza kwenye miradi  mbalimbali ya maendeleo na kueleza kuwa huko nyuma ilikuwa ni changamoto kupata huduma kwa wakati tofauti na hivi sasa ambapo wamesogezewa kwa ukaribu.

Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa amesema Serikali imewekeza  miundombinu ya maendeleo vijiji vingi vya wilaya hiyo ya Kongwa vina umeme,shule,vituo vya afya na barabara zenye kupitika kirahisi kwa kipindi chote na kuimarisha mawasiliano ya simu na hivyo kirahisisha maendeleo.

"Hili la mawasiliano ya mitandao vijiji vingi vilikuwa hakuna mawasiliano,lakini kwa hivi sasa serikali imeadhimia kujenga minara 10 yenye uwezo mkubwa na wananchi wanaenda kuondokana na kero ya kukosa mawasiliano"amesema.


Naye Kanoni Ndatila amesema,"Tunamshukuru mbunge kupitia serikali yetu ndani ya kipindi chake tumeona jitihada ambazo zimefanyika ikiwemo miundombinu ya elimu afya umeme kilimo ma barabara ambazo hivi sasa zinapitika kwa muda wote"amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post