WASAFIRISHAJI WA VIFURUSHI NA VIPETO NYANDA ZA JUU KUSINI WATAKIWA KURASIMISHA HUDUMA ZAO


Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John akuzungumza na Watoa Huduma za Vifurushi na Vipeto (Hawapo pichani)kuhusiana na kujisajili na kuwa leseni ya biashar hiyo katika mkutano uliofanyika mkoani hapa Mbeya .

*Ni Kampeni ya TUMA CHAP ya TCRA

Na Mwandishi Wetu Mbeya

Wasafirishaji wote wa vifurushi na vipeto wanaofanya kazi katika kanda ya nyanda za juu kusini yametakiwa kutumia muda huu wa upendeleo kurasimisha huduma zao za usafirishaji kwa kuchukua leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za Kiposta Mkoa wa Mbeya Meneja wa TCRA kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema umiliki wa leseni ya TCRA unaongeza mapato kwa watoa huduma kwani wateja wengi wanavutiwa zaidi kutuma mzigo kwa watoa huduma rasmi na kuondoa usumbufu namna ya upatikanaji wakati anahitaji kutuma kifurushi/Kipeto.

Amesema kuongezeka kwa wateja kunapelekea kuongezeka kwa mapato ya watoa huduma ambayo yanachangia ongezeko la pato la taifa.

Mhandisi Asajile amesema ili kufanikisha hilo TCRA imeanzisha mfumo wa utoaji leseni mtandaoni ujulikanao kama mfumo wa Tanzanite ambapo mtoa huduma anaweza kuomba hadi kupata leseni kwa njia ya mtandao jambo ambalo linarahisisha utendaji na kuokoa gharama.

Ameongeza kuwa iwapo waombaji hao wa leseni watakumbana na changamoto katika kuombq leseni wanaweza wasiliana na TCRA kupitia namba ya dawati la huduma ambayo ni 0800008272 au kufika katika ofisi yoyote ya Mamlaka kwa msaada zaidi.

Mkutano huu ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutumia huduma za watoa huduma wa kusafirisha vifurushi waliosajiliwa ijulikanayo kama TUMA CHAP kwa usalama ambapo inahusisha kuhamasisha watoa huduma wajisajili na jamii kuwatumia watoa huduma rasmi.
Picha ya pamoja ya Meneja wa TCRA Kanda za Nyanda za Juu Kusini Mhandiso Asajile John akiwa katika picha ya pamoja watoa huduma za usafirishaji wa Vipeto na Vifurushi, mkoani Mbeya

Baadhi ya Wadau wakufatilia mada kuhusiana na kujisajili na kupata leseni za usafirishaji wa vipeto na vifurushi.

Afisa Habari na Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kuhusiana na Kampeni ya Tuma Chap ya TCRA katika Mkutano wa Wadau mkoani Mbeya.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post