Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akisisitiza jambo kwa wadau mbalimbali wakati akifungua kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, Msingi, Sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe,,akizungumza wakati wa kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, Msingi, Sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Prof.Kitila Mkumbo ,akizungumza wakati wa kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za mkoa wake wakati wa kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani),wakati akifungua kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mitaala Prof.Makenya Maboko,akitoa wasilisho la kwanza kutoka kamati ya mabadiliko ya Mitaala wakati wa kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akifatilia mawasilisho mbalimbali kutoka kwenye Kamati ya Mapitio ya Sera na Kamati ya mabadiliko ya Mitaala wakati wa kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika jijini Dodoma kuanzia leo Mei 12-14, 2023,mwaka huu.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda ,amewataka wadau kutoa maoni kwa uwazi kwenye rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo na Mitaala toleo 2023, zinazolenga kuleta mageuzi makubwa na kuongeza ubora wa elimu nchini.
Waziri Mkenda ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la kujadili sera na mitaala mipya ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu linalofanyika kuanzia leo Mei 12-14, 2023 jijini Dodoma.
Prof.Mkenda Amesema kongamano hilo limekutanisha wadau mbalimbali wakiwamo watanzania kutoka ughaibuni. “Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kufanya mageuzi makubwa yanayozingatia matakwa ya wananchi mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya sasa na baadae katika mazingira ya utandawazi,”amesema Prof.Mkenda
Aidha amesema kuwa mageuzi hayo yanalenga kuwezesha wahitimu kuwa na ujuzi na kujiamini ili kujiajiri na kuajirika. “Ni matumaini yangu kuwa mtatoa maoni na ushauri ambao utakuwa chachu ya maboresho ya rasimu ya elimu na mafunzo na mitaala mipya ya elimu,”amesisitiza.
Hata hivyo amesema kuwa Serikali imedhamiria kufufua na kurudisha shule za sekondari na ufundi ambazo zitaanza kuchukua wanafunzi kuanzia Januari mwakani.
Prof. Mkenda amesema kuwa mapendekezo ya kufufua shule za sekondari za ufundi ni kutokana na vijana wengi kuona kama kusoma ufundi bila kuwa na elimu ya sekondari ni kujidhalilisha .
“Tumetenga bajeti ya kurudisha shule zetu za sekondari ambazo pia zinafundisha masomo ya ufundi ,hii ni kwa sababu tumeona vijana wengi wakienda kusoma katika vyuo vya ufundi,wanarudi tena kufanya mtihadi wa kidato cha sita ili waende vyuo vikuu,wakidhani kusoma ufundi ni kujidhalilisha.”amesema Prof.Mkenda
Aidha Waziri Mkenda amewatoa hofu walimu waliopo kazini,tutakapoanza utaratibu mpya wa kupata walimu ,wao hautawahusu na wataendelea na kazi mpaka watakapostaafu na badala yake Serikali itaangalia namna ya kuwapa nafasi ya kwenda kujiendeleza kielimu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof.Carolyne Nombo, amesema mapitio ya mitaala kwa vyuo vya ufundi na elimu ya juu nayo yameanza vizuri kwa lengo la kuoanisha na elimu inayotolewa katika ngazi za elimu zinazoanza.
''Katika utekelezaji wa rasimu hiyo kulikuwa na kmati mbili ambazo zimefanya kazi ya kukusanya maoni ambapo zaidi ya wadau 200,000 walifikiwa na kupata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu maboresho ya sera na mitaala ya elimu hapa nchini.''amesema Prof.Nombo
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Prof.Kitila Mkumbo,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kufanya mageuzi hayo ya elimu nchini kwa kuwa kilikuwa kilio cha muda mrefu cha kupitia mfumo wa elimu.
''Kongamano hilo ni fursa kwa wabunge kuchukua maoni na kuyafanyia kazi ili kuhakikisha serikali inayachukua lakini pia kwa yale ya kisheria,Kamati hiyo itahakikisha Sheria inatungwa.''amesema Prof.Mkumbo
Aidha Prof.Mkumbo amempongeza Waziri Mkenda na timu yako ya wizara kwa kuwa wepesi kufanyia kazi maelekezo ya Rais ya kupitia sera na mitaala, duniani kote elimu ina mambo matatu, fursa, ubora wa elimu na elimu itolewayo kuwasaidia wanaoipata kujitegemea.