****************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga inefanikiwa kutinga Fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 (agg-4-1) dhidi ya timu ya Marumo Gallants ambapo mchezo wa mkondo wa kwanza Yanga akiwa nyumbani alipata ushindi wa mabao 2-0.
Katika mchezo huo ambao Yanga Sc iliweza kuwapumzisha baadhi ya wachezajj wake akiwemo Aziz Ki pamoja na Moloko ambao wote walianza kwenye mchezo uliopita mkondo wa kwanza.
Yanga Sc ilianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Fiston Kalala Mayele akipokea pasi nzuri kutoka kwa Kenned Musonda na kuzamisha moja kwa moja wavuni na kuwatanguliza mbele 1-0.
Kipindi cha pili Yanga Sc iliendelea kulisakama lango la mpinzani kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo walishindwa kuzitumia ingawa jitihada za Mayele zilisaidia na kuweza kuoata bao la pili kupitia kwa Musonda, goli lililotengenezwa na Fiston Mayele.
Kwa ushindi huo mnono wa Yanga Sc inawafanya kuweka historia kutonga Fainali kwenye historia ya Mpira wa Miguu Tanzania.
Yanga Sc imetangulia Fainali kwa jumla ya Mabao 4-1 hivyo wataisubiri kati ya USM Alger na ASEC Mimosas ambao wanacheza baadae.
Social Plugin