Mahakama nchini Uganda imemuamuru msimamizi wa WhatsApp wa kundi moja kumrejesha mwanachama aliyemshtaki kwa kumfukuza kwenye kundi hilo.
Mwanaume mwenye hasira kutoka Uganda aliyetambulika kwa jina la Herbert Baitwababo alikwenda mahakamani kuwashtaki wasimamizi wa kundi la WhatsApp la 'Buyanja My Roots' kwa kumuondoa kwenye kundi hilo baada ya kuuliza maswali kuhusu utumizi wa pesa walizokuwa wamechanga.
Katika ripoti ya gazeti la Daily Monitor, Herbert, kwenye stabadhi za mahakama, alisema shida ilitokea wakati alipoanza kuuliza jinsi ukaguzi na uwajibikaji wa fedha zilizochangwa kwenye kundi la WhatsApp.
Wanachama walikuwa wakichanga KSh 1,000 kama ada ya uanachama, na kundi hilo lilikusudiwa kusaidia kazi za hisani, lakini alipouliza kuhusu jinsi pesa hizo zilivyotumika, alifukuzwa.
Mnamo Jumatatu, Juni 19, 2023 Herbert alipata ahueni baada ya mahakama kwamba kufukuzwa kutoka kwa kikundi cha WhatsApp ni kinyume na uhuru wake wa kujumuika.
"Agizo la kudumu pia limetolewa kumzuia mlalamikiwa, mawakala wake au wasaidizi wake kuendelea kukiuka haki ya ushirika ya mwombaji," alisema hakimu.
Social Plugin