Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine 8 kujeruhiwa baada ya Magari matatu kugongana katika eneo la Kingolwira manispaa ya Morogoro barabara ya Dar es salaam Morogoro.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo ambapo gari moja lililobeba mafuta ya Petrol lililokuwa likitokea Dar es laam kuelekea Morogoro liligongana na basi la abiria la Johanvia lililokuwa likitokea Musoma kuelekea Dar es salaam na kisha basi hilo kuligonga gari la Polisi lililokuwa limepaki pembeni mwa barabara.
Kamanda Mkama amemtaja aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni Yohana Mwamlima( 40) aliyekuwa akitokea Musoma kwenda Dar es salaam.
Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari la mafuta ambaye alikuwa anaendesha gari hilo kwa mwendo kasi.
Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mkoa wa Morogoro amethibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja na majeruhi 8 wakiwemo wanaume 5 na wanawake 3.
Social Plugin