Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA RIPOTI ZA CAG

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania – NAOT) imetoa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) ambapo waandishi wa habari wamejengewa uwezo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo nafasi ya Vyombo vya habari katika kuandika ripoti za ukaguzi wa mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aina za ripoti za ukaguzi pamoja na Sheria , Taratibu na Kanuni zinazosimamia uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Akifungua mafunzo hayo leo Jumatano Juni 28,2023 kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (AAG), Anna Massanja amesema Vyombo vya habari ni miongoni mwa wadau muhimu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi vikiwa na jukumu la kuandika habari, makala na uchambuzi kuhusu Ripoti za ukaguzi wa CAG na taarifa za jumla za CAG, kuibua masuala muhimu ambayo yanaweza kuchunguzwa na ambayo yanaweza kupelekea ukaguzi maalum.

Amesema pia vyombo vya habari hutoa taarifa kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na serikali katika kutekeleza mapendekezo ya CAG pamoja na kuelimisha wananchi kuhusu majukumu ya CAG ili kuendeleza uwajibikaji nchini.
Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (AAG), Anna Massanja 

“Tunatambua na kuheshimu mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari katika kuelimisha umma, jambo ambalo limesababisha jamii kuendelea kufahamu na kutambua umuhimu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi”, amesema Massanja.

“Hii siyo mara ya kwanza Ofisi ya Taifa ya ukaguzi kufanya mafunzo ya aina hii kwa Waandishi habari, kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukiendesha mafunzo ya aina mbalimbali kwa Wahariri na Waandishi wa habari kutoka maeneo mengine na mafunzo haya yatakuwa endelevu,”ameongeza Massanja.

Aidha amewahimiza Waandishi wa habari kuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya fedha za umma, na kujifunza kuhusu mifumo ya bajeti, taratibu za manunuzi na sheria zinazosimamia matumizi ya fedha za umma, ujuzi ambao utawawezesha kufanya uchambuzi bora na kutoa taarifa sahihi kwa umma.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa waandishi habari kutambua kwa upana shughuli za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa nje wa hesabu za Serikali, ili kuisaidia jamii kupata uelewa kupitia habari na kufuatilia rasilimali zao kwa ajili ya maendeleo.

“Naipongeza Ofisi ya Taifa ya ukaguzi kwa kutupatia mafunzo haya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga kwa mara ya kwanza, ambayo yametujengea uwezo namna ya kuripoti habari zetu kwa ufanisi, na kuibua habari za usimamizi wa fedha”,amesema Kakuru.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (AAG), Anna Massanja akitoa hotuba wakati ufunguzi wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania – NAOT). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (AAG), Anna Massanja akitoa hotuba wakati ufunguzi wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania – NAOT).

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza wakati wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania – NAOT).

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Shinyanga Patric Lugisi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi Idara ya Sheria kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania – NAOT),  Elieshi Saidimu akiwasilisha mada wakati wa mafunzo

Mkaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania – NAOT),  Hagai Maleko akiwasilisha mada wakati wa mafunzo

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (National Audit Office of Tanzania – NAOT),  Focus Mauki akiwasilisha mada wakati wa mafunzo

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Patrick Mabula akizungumza wakati wa mafunzo

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com