Msanii maarufu wa nyimbo za utamaduni wa kikundi cha Shinyanga Arts Group Fadhili Mungi maarufu Chap Chap (44) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Juni 30,2023 jijini Dar es salaam.
ChapChap alikuwa anasumbuliwa na tatizo la Kansa katika mfumo wa hewa kwa muda mrefu na hivi karibuni alifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa za awali zinasema mazishi yatafanyika kesho Chang'ombe Kisarawe.
R.I.P Fadhili Mungi
Social Plugin