Imeelezwa kuwa kuchelewesha malipo Kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wanaotoa Huduma katika migodi kunachangia kuzorotesha mzunguko wa Biashara za wajasiriamali pamoja na kuishiwa mitaji ya kuendeleza biashara zao.
Hayo yamebainika leo katika warsha ya kutoa matokeo ya ripoti ya Utafiti wa ushirikikishwaji wa wazawa Kwenye sekta madini Tanzania iliyofanyika katika mkoa wa Mara na Geita.
Akitoa taarifa ya Utafiti huo Afisa ufuatiliaji,Tathimini na mafunzo Kutoka Hakirasilimali Francis Mkasiwa amesema kuhusu Hali ya ajira kwa wazawa Utafiti unaonyesha kuwa wazawa wanapewa kazi za kuuza mbogamboga,Huduma za usafiri,malazi,kuuza Chakula na kuuza vifaa vya ujenzi.
Francis ameongeza kuwa tafiti waliofanya inaonyesha watoa Huduma hawalipwi fedha zao Kwa wakati Hali inayokwamisha mzunguko wa Biashara zao pamoja na kuishiwa mitaji Yao.
Sambambam na hayo ripoti inaonyesha kuwa Hali ya kuhamisha maarifa Kwa wazawa ni ndogo kwani elimu na mafunzo hutolewa Kwa Watu wachache na yasiyo ya kudumu Kwa wazawa hao.
Awali akifungua warsha hiyo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mtandao wa mashirika yanayofanya kazi katika sekta ya madini na Gesi (Hakirasilimali) Jimmy Luhende amependekeza kuendelea kufanyika tafiti nyingi za kisayansi katika migodi inayozunguka wananchi ili kunufaisha pande zote za wawekezaji na wananchi.
Nao baadhi ya washiriki wa warsha hiyo Bonny Matto Kutoka tarime na Asia Hussein Kutoka Gieta wamewashauri viongozi hususa wenyeviti na madiwani kutetea na kusimamia sheria ndogo Ili kuwe na manufaa ya pamoja kati ya wananchi na wawekezaji.
Akitoa ufafanuzi kuhusu ucheleweshaji wa malipo Kwa watoa Huduma Meneja mahusiano wa AKO GROUP LTD Waisile Bairi amesema utaratibu wa malipo Huwa unafanyika ndani ya siku thelathini baada ya mtoa Huduma Kupeleka Ankra (Invoice) Kwa mwekezaji.
Warsha hiyo ya Siku moja iliyofanyika Mkoani Geita ya uzinduzi wa ripoti ya Utafiti wa Ushirikikishwaji wa wazawa Kwenye sekta ya madini iliyoandaliwa na Hakirasilimali na Policy Forum imejumuisha wadau wa madini Kutoka mkoa wa Mara,Shinyanga na Geita.
Social Plugin