Katika ulimwengu ambapo harusi za kifahari zenye mamia ya wageni zimekuwa jambo la kawaida, mwanaume mmoja amejitokeza kwa ujasiri kuchukua hatua tofauti.
Bwana harusi mtarajiwa amezua gumzo kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuamua kuwaalika watu watatu tu katika harusi yake.
Kulingana na Mirror, katika kile kinaonekana kuwa ni hali ya kawaida ya kuwa na sherehe ya faragha, suala hilo limegeuka kuwa mjadala mkali mtandaoni ambao umevuta hisia za maelfu ya watu.
Bila kuyumba katika azimio lake, mwanaume huyo aliamua kutumia Reddit kutafuta ushauri na msaada.
Alikiri kuwa uamuzi wake usio wa kawaida ulisababisha migawanyiko kati ya marafiki zake. Hali hiyo ilichukua mkondo usiotarajiwa pale ambapo msimamizi wake ambaye ni rafiki wa karibu, alitishia kutohudhuria harusi hiyo iwapo mpenzi wake atajumuishwa kwenye orodha ya wageni.
Alisema: "Mchumba wangu na mimi tunataka kufunga ndoa mwaka huu. Hatupendi harusi za kawaida na hatupendi kuwa kitovu cha matakwa ya watu. Tunataka kufunga ndoa hasa kwa ajili yetu kwa sababu tunapendana, si kwa ajili ya watu wengine."
"Tumekubaliana kuwa kila mmoja wetu ataalika mtu mmoja tu (bwana harusi na bibi harusi wa heshima). Kim, rafiki mzuri wa bibi harusi, pia atakuja kwa sababu yeye huchukua picha na sisi wote tunamjua vizuri. Kwa jumla, kutakuwa na watu watano tu. Hiyo ndiyo yote."
Bwana harusi mtarajiwa alibainisha kuwa hawataki watu wengine zaidi katika siku yao maalum na baadhi ya wanafamilia hawajaalikwa. "Tumefikiria sana katika kuchagua watu watatu. Hata familia zetu hazijaalikwa."
Social Plugin