Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMBO FM YAZINDULIWA RASMI...RC MNDEME AIPONGEZA KWA KAZI KUBWA YA KUHABARISHA UMMA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme ameipongeza Jambo FM inayorusha matangazo yake kutoka katika Manispaa ya Shinyanga kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhabarisha, kuelimisha na kurudisha umma kupitia masafa ya 92.7 MHz.


Mhe. Mndeme ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kituo hicho cha Redio tukio ambalo lilitanguliwa na mazoezi ya Jogging kutoka SHY COM mpaka VETA na kurudi hadi eneo la NBC Mataa ambapo alishriki zoezi la kupanda miti eneo hilo ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa kituo sambamba na kutunza mazingira katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwaahidi kuwapatia ushirikaino wakati wote.


"Nawapongeza sana Jambo FM na Jambo Food Products kwa ujumla kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa wananchi wa Mkoa huu wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla wake ya kuhabarisha umma, kuelimisha na kuburudisha huku Jambo Food Product mkizalisha ajira kwa wananchi pamoja na kukuza uchumi kwa wananchi na kuongeza pato la Taifa, hongereni sana Jambo," alisema Mhe. Mndeme.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi alisema kuwa, Jambo FM wamekuwa wadau muhimu sana wakati wote katika utekelezaji wa kazi za habari kwa maeneo haya huku akiwataka kuendelea na utamaduni huu kwa maslahi mapana kwa wananchi.


Kwa upande wake Meneja wa Jambo FM Redio Ndg. Nickson George alimuambia mgeni rasmi kuwa, Jambo FM wamefurahi sana kwa kukubali kwake Mhe. Mndeme kuwa mgeni rasmi katika tukio hili la ufunguzi wa Redio na kwamba hii ni ishara tosha kwamba Serikali inafanya kazi na Jambo FM pamoja na Jambo Food Products huku akimuahidi kuendelea ushirikiano na Serikali wakati wote kwa weledi na kuzingatia maadil.


Jambo FM na Jambo Food Product leo wamefanya ufunguzi wa kituo cha Redio ambapo pamoja na mambo mengine pia wamefanya tamasha kubwa la burudani katika viwanja vya SHY COM tukio ambalo limejumuisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, ngoma za asili na michezo mbalimbali ijulikanayo kama SIKUKUU JAMUKAYA kauli mbiu "Tunakula Bata la Mafanikio".







NaShinyanga RS.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com