John Anthony,miaka 21, mkazi wa kijiji cha Nanga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu amehukumiwa kifungo cha Maisha Jela baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 13.
Hukumu hiyo imesomwa tarehe 19.06.2023 na Mh. Robert Kaanwa Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Edith M. Swebe ACP akizungumza na vyombo vya habari leo hii, ameleeza kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 10/02/2023 huko katika kijiji cha Nanga Wilaya ya Itilima Mkoa wa Simiyu ambapo mtuhumiwa John Anthony alimbaka na kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo.
Toka Dawati la Habari Simiyu
Social Plugin