Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MABASI YA KATARAMA NA ALLY'S BUS YAFUTIWA RATIBA YA SAA 9 ALFAJILI... MASHABIKI STENDI WAWAPONZA KUMWAGIA MAJI

LATRA imeyafutia magari sita ya Ally's Star na matatu ya Katarama Express kufanya safari zake za kusafirisha abiria kuanzia saa 9:00 usiku na badala yake yatapaswa kuanza safari zake saa 12:00 asubuhi kuanzia Jumatano Juni 21, 2023, baada ya kugundulika yamekuwa yakishindana kufika katika vituo vya mabasi na kwamba basi lililoshinda lilimwagiwa maji na kushangiliwa.

Mabasi hayo ni sita (6) ya Ally's Star (T946 EBF, T947 EBF, T948 EBF, T354 DXS, T357 DXS na T360 DXS) na matatu (3) na Katarama Express (T835 EBR, T836 EBR, T212 ECR) na endapo wataendelea kukiuka maelekezo leseni zao zitafutwa.

Aidha kampuni ya Isamilo, kwa kuwa matukio yake hayajakithiri, pamoja na watoa huduma wengine wanaofanya mchezo huu, wamepewa onyo kali na la mwisho kabla hawajachukuliwa hatua stahiki.

Mbali na hayo madereva na wamiliki wa magari wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utoaji huduma za usafiri wa umma.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com