Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AKATWA MKONO KISA MADENI


Picha haiendani na tukio

Mwanaume mmoja anauguza majeraha mabaya katika hospitali ya kaunti ndogo ya Nyambene nchini Kenya ambapo amekimbizwa baada ya kushambuliwa na rafiki yake.


Kwa mujibu wa polisi, mkutano wa Johanna Grison mwenye umri wa miaka 45 na rafiki yake uliishia katika mapigano ambayo yalipelekea mkono wake kukatwa.


Katikati ya ugomvi huo kulikuwa na KSh 10 (170Tsh) ambazo polisi walidai Johanna alikuwa anadaiwa na rafiki yake, Murithi Njeru mwenye umri wa miaka 35.


Inasemekana Njeru alimwomba pesa zake kutoka kwa Johanna ambaye hakuweza kumpa mara moja.


Akiwa amekasirika, Njeru aliondoa panga ambalo aliripotiwa kukata mkono wa kushoto wa Johanna kabla ya kukimbia.

Watu wema waliposikia kilio chake cha uchungu, walimsaidia na kumpeleka kwenye kituo cha Polisi cha Kanjoo.

"Baadaye alitolewa katika eneo la tukio na msamaria mwema pamoja na sehemu iliyokatwakatwa na kusindikizwa hadi polisi," taarifa ya polisi ilidokeza.




Johanna anasemekana kukiimbizwa hospitalini baada ya kurekodi taarifa ya uvamizi huo kwenye kituo cha polisi.




Tukio hilo liliandikishwa chini ya OB 05/14/06/2023 huku wachunguzi wakianza kumfuatilia mshukiwa.




Katika kisa sawia, marafiki wawili waliaga dunia hivi majuzi baada ya vita kuzuka kati yao mjini Nyeri ambapo walikuwa wanazozania KSh 20.




Via: Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com