Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA BIASHARA MATATANI KWA KUWAITA WAANDISHI WA HABARI 'MAKAHABA"


Waziri wa Biashara wa nchini Kenya, Bwana Moses Kuria picha na mtandao.


Na Sute Kamwelwe - Kenya.
Muungano wa Wanahabari wa Kenya (KUJ) pamoja na Kamati ya kuwalinda wanahabari barani Afrika (CPJ) imemjia juu Waziri wa Biashara wa nchini Kenya, bwana Moses Kuria baada ya kutishia na kutoa matamshi tata kwa waandishi wa habari wa kampuni ya Nation Media Group (NMG) akiwaita ‘makahaba’.

Sakata la kuwashambuliwa wanahabari hao liliibuka siku chache baada ya Televisheni ya NTV inayomilikiwa na kampuni ya NMG kutoa taarifa ya uchunguzi inayoonyesha kashfa ya mpango wa uagizaji mafuta ya kupikia bila ushuru unaoendeshwa na shirika la serikali.

Kuria alitoa kauli hiyo isiyo ya kiungwana baada ya maofisa wa Serikali hiyo kuendelea kushirikiana na NMG katika matangazo ya vyombo vya habari huku akiwatishia kuwafukuza kazi endapo wakiendelea.

Aidha, waziri huyo alihoji kama chombo hicho cha habari kipo kwa ajili ya kutoa taarifa au chama cha upinzani. 

Siku inayofuatia Juni 18, Kuria alienda mbali zaidi na kuwatishia maofisa hao kuwafuta kazi serikalini.

Katika mfululizo wa tweets kati ya Juni 18 na Juni 20, Kuria aliwaita wafanyakazi wa kampuni hiyo ‘makahaba,’ akiwashutumu kwa rushwa na upendeleo, na kuahidi kuchapisha majina ya waandishi ambao wamekiri kulazimishwa kuandika kinyume habari za serikali.

Chanzo - Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com