Fedha zilizokuwa zimeibiwa
Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara, linamshililia Gifti Fredrick (22) kwa tuhuma za wizi wa shilingi milioni 21 za mmoja wa wafanyabiashara wa mji mdogo wa Mirerani na baada ya kuziiba fedha hizo alizichimbia chini ya ardhi.
Gifti amekamatwa Juni 18, 2023, katika mtaa wa Kangaroo, akiwa na fedha kiasi cha shilingi milioni 19.7 alizokuwa amezichimbia chini, licha ya kwamba kiasi halisi alichokuwa amekiiba ni milioni 21
Ni mara ya tatu sasa kwa Jeshi la Polisi Manyara kuokoa mamilioni ya fedha za wafanyabiashara
Awali Jeshi hili liliokoa kiasi cha Sh20 millioni za mfanyabiashara mjini Babati kisha kuokoa tena Sh 47 millioni za mfanyabiashara mwingine wa mji mdogo Mirerani na leo kiasi cha Sh21 millioni za mfanyabiashara mwingine zimeokolewa.
Chanzo - EATV
Social Plugin