Mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Busia nchini Kenya amemuua nyanya yake kwa kumdunga kwa kisu katika kijiji cha Kisoko eneo bunge la Nambale.
Kwa mujibu wa familia, Bernard Okwara mwenye umri wa miaka 25 alimshambulia na kumuua Clare Oruko mwenye umri wa miaka 96 ambaye alikuwa katika jikoni yake.
Kufuatia kisa hicho, majirani na jamaa zake walinasa mshukiwa na kumfunga kwenye mti kabla ya kuwaita maafisa wa polisi.
Mshukiwa ni mwalimu katika shule ya upili ya Nanderema katika kaunti ndogo ya Samia.
Familia inasema kuwa amekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja kaunti ya Kakamega kwa matatizo ya akili.
Mwili wa mwendazake umepelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Busia huku mshukiwa akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Nambale.
Social Plugin