Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI SHINYANGA WAKAMATA WATUHUMIWA 19, BUNDUKI & DAWA ZA KULEVYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watuhumiwa 19 kwa kujihusisha na matukio ya uhalifu huku likifanikiwa kukamata vitu na vielelezo mbalimbali ikiwemo silaha aina ya Chinese Pistol yenye namba 071T4823 ikiwa na risasi tano, pikipiki 4, baiskeli 2 na mafuta aina ya Diesel lita 60 na Petrol lita 20.


Vitu vingine ni Dawa za kulevya aina ya Bangi kilo 60 na gramu 540, Mirungi bunda 58, Heroine kete 166, Television 2, Godoro 1, Subwoofer 1 na CPU 1.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari leo Jumatano Juni 21,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema watuhumiwa hao na vitu hivyo vimekamatwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 28/05/2023 hadi tarehe 21/06/2023 kupitia misako na doria mbalimbali.


Ameeleza kuwa katika kipindi hicho kesi mbalimbali ziliweza kufanikiwa mahakamani ikiwemo kesi moja ya mauaji ambapo mtuhumiwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, kesi moja ya kujaribu kubaka ilihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na nyingine mbili za kubaka zilihukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kila moja.


“Pia kesi moja ya kumpa mimba mwanafunzi mtuhumiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela na kesi moja ya kutorosha mwanafunzi ilihukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela”,amesema Kamanda Magomi.

Amezitaja kesi zingine zilizopata mafanikio ni pamoja na kujeruhi ambayo ilihukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela, kujifanya mtumishi wa Serikali miaka 02 Jela, kuvunja nyumba usiku ilihukumiwa miaka 05 Jela na wizi wa gari ilihukumiwa miaka 03 Jela.


Kwa upande wa Usalama barabarani, Kamanda Magomi amesema Jumla ya makosa 3,352 yalikamatwa na kulipiwa fine, lakini pia madereva wawili wa mabasi wamefungiwa leseni zao kwa kukiuka taratibu za usalama barabarani.


“Tunazishukuru na kuzipongeza idara za mahakama na mwanasheria wa serikali kwa kuhakikisha adhabu kali zinatolewa kwa wale wote wanaopatikana na hatia kwa vitendo mbalimbali vya kihalifu. Pia tunawashukuru wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano mzuri na Jeshi la Polisi na tunawaomba waendelee kutoa ushirikiano zaidi ili kudumisha amani na usalama uliopo”,ameongeza Kamanda Magomi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Juni 21,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Juni 21,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Juni 21,2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha silaha aina ya Chinese Pistol 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha silaha aina ya Chinese Pistol ikiwa na risasi tano
silaha aina ya Chinese Pistol na risasi tano
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha bangi iliyokamatwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mirungi iliyokamatwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali mbalimbali zilizokamatwa 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha mali mbalimbali zilizokamatwa 
Mali mbalimbali zilizokamatwa 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com