Taarifa za kuhuzunisha zilizotufikia kwenye chumba chetu cha habari zimeeleza kuwa, mmiliki wa Kampuni ya Ndege ya Precision Air, Michael Ngaleku Shirima amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa, Mzee Shirima amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 10, 2023 alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini jijini Dar es salaam.
Imeelezwa kwamba Mzee Shirima alilazwa hospitalini tangu Juni 8, 2023.
Kifo cha Mzee Shirima kimethibitishwa na Kampuni ya Precision Air.
Social Plugin