Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Walter Kaaya (34) mkazi wa Simanjiro mkoani Manyara amenusurika kifo kwa kupigwa risasi na Paulo Laizer (43) mfugaji wilayani humo kufuatia mzozo wa mifugo kukutwa shambani ikiharibu mazao.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amesema majeruhi alikuwa akiondoa ng'ombe hizo kwenye shamba lake la ekari 200 zilizokuwa na mazao mbalimbali yakiweno mahindi na maharagwe
Wakati anaziondoa ng'ombe shambani mtuhumiwa alifika na kuibua mzozo na kuchukua silaha yake aina ya bastola na kumpiga risasi begani
Majeruhi amekimbizwa katika hospitali ya KCMC Moshi kwa matibabu zaidi.
Chanzo - EATV
Social Plugin