Kaimu Mkurugenzi SHUWASA Mkoa wa Shinyanga Sarah Emmanuel akizungumza na waandishi wa habari leo June 30 2023 katika ukumbi wa mikutano SHUWASA.
Na Halima Hoya,Shinyanga.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imetoa taarifa taarifa yake ya utekelezaji wa majukumu yake katika kuwahudumia wananchi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 huku ikiahidi kufanya maboresho zaidi Tinde,Didia,Shinyanga Manispaa na Iselamagazi.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Juni,30,2023 Kaimu Mkurugenzi SHUWASA Mkoa wa Shinyanga Sara Emmanuel amesema Zaidi ya Bil. 1.6 zinatumika kutekeleza miradi hiyo ambapo fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji.
Emmanuel amesema kuwa miradi hiyo ni Pamoja na ujenzi wa mtandao wa Bomba za usambazaji lenye takribani kil.8.1 kwa awamu ya kwanza utakaohudumia vijiji vya Jomu na Nyambui ambapo ujenzi huo ni mwendelezo wa ujenzi wa mradi wa Tinde-Shelui uliotekelezwa na Wizara ya Maji na kutumia Zaidi ya Bil.24.47 kukamilisha ujenzi wake.
“Kwa sehemu ya Tinde mradi uligharimu kiasi cha sh.5.22 na utekelezaji wake ulianza rasmi 21.08.2023 ukiwa umesainiwa kuhudumia Zaidi ya wananchi 600,000 kutoka katika vijiji 22 na kuhusisha kazi ya ulazaji wa Bomba,ujenzi nwa tenki la maji safi na ukarabati wa tenki moja Didia”amesema Emmanuel.
Hata hivyo miradi mingine ni Pamoja na Tanki la Didia,Iselamagazi na mradi wa majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na kwamba SHUWASA inaendelea na maandalizi ya nyaraka mbalimbali za mradi ikiwa ni pamoja na kuhusisha vibali kwa hatua kutoka kwa mfadhili.
Nae Kaimu Meneja Kanda ya Tinde SHUWASA Joshua Yohana, amesema Mradi huu umetekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ni ujenzi wa tanki la maji na awamu ya pili ni ujenzi wa bomba la kusambaza maji Kwenda kwa wakazi Zaidi ya vijiji 22 ambapo wameanza na vijiji vitatu (Nyambui,Jomu na Buchama).
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi waliofikiwa na huduma hiyo,Alexandra Masele na Elizabeth wamesema mradi huo umesaidia kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji sambamba na kununua maji kwa gharama kubwa.
Kaimu Mkurugenzi SHUWASA Mkoa wa Shinyanga Sarah Emmanuel akizungumza na waandishi wa habari leo June 30 2023 katika ukumbi wa mikutano SHUWASA.
Kaimu Mkurugenzi SHUWASA Mkoa wa Shinyanga Sarah Emmanuel akizungumza na waandishi wa habari leo June 30 2023 katika ukumbi wa mikutano SHUWASA.
Afisa Uhusiano na Mahusiano kwa Umma Nsianel Gerald akiwa kwenye kikao na waandishi wa habari kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano SHUWASA.
Kaimu Meneja Kanda ya Tinde SHUWASA Joshua Yohana akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara Tinde.
kifaa cha kuunganisha maji.
Social Plugin