Watu watano waliofariki baada ya chombo cha Titan kupoteza mawasiliano na mabaki yake kuonekana mita chache na yalipo mabaki ya Meli ya Titanic chini ya Bahari ya Atlantiki.
Kwa upande wa kampuni ya OceanGates imesema kuwa, "Sasa tunaamini kwamba Mkurugenzi Mtendaji wetu Stockton Rush, Shahzada Dawood na mwanawe Suleman Dawood, Hamish Harding, na Paul-Henri Nargeolet, wameaga dunia".
Aidha roboti ya ROV kutoka Meli ya Horizon Artic ilipata mabaki matano tofauti ya chombo hicho cha chini ya maji (Submarine) ikiwemo pua na mkia wa chombo hicho cha Titan pamoja na sehemu ya chemba ya presha ya chombo hicho.
Kifaa kilichokuwa kimewabeba watu hao watano
Walinzi wa Pwani ya marekani wamesema kwamba wataendelea kuchunguza eneo la bahari ambako mabaki ya chombo hicho yamepatikana ikiwa ni mita chache tu na yalipo mabaki ya Meli ya Titanic iliyozama mwaka 1912.
Chombo hicho (Submarine) kilipoteza mawasiliano siku ya Jumapili ikiwa imepita saa 1:45 tangu kianze safari yake ya kupeleka watalii chini ya bahari mita 3,800 yanakopatikana mabaki ya Meli ya Titanic.
Kampuni ya OceanGate huwatoza wageni $250,000 sawa na takribani milioni 500 za Kitanzania katika msafara wake wa siku 8 ili kuona mabaki ya Meli hiyo ambayo iko mita 3,800 chini ya usawa wa Bahari ya Atlantiki.
Social Plugin