Makamu wa Askofu Mkuu wa AICT Askofu Zakayo
Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania,
Dayosisi ya Shinyanga leo amefungua semina ya idara ya wanawake wa kanisa la AICT ambayo
itafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa chuo cha ualimu SHYCOM mjini
Shinyanga.
Askofu Bugota ametumia nafasi hiyo
kuwakumbusha kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine katika
juhudi za kukemea mmomonyoko wa maadili, tabia na destori kandamizi pamoja na
migogoro ya ndoa na familia.
Askofu Bugota Amesema kuwa ipo haja ya wanawake wakanisa hilo kuendelea kushirikiana ili
kuhakikisha wanapaza sauti ya pamoja kukemea tabia zinazokwenda kinyume na
maadili ikiwemo mavazi yasiyo na staha.
Ipo changamoto ya ndoa za masafa ambazo nindoa unakuta mwanaume anafanya kazi mkoa tofauti na mkoa anapo fanyia kazi mwenza wake hili ni tatizo ambalo kwa kiasi kikubswa linachangia migogoro katika familia.
“changamoto kama hii ya ndoa za masafa inahitaji mkakati wa pamoja utakao saidia kupunguza changamoto hiyo katika jamii yetu”.
“Kuna migogoro ya ndoa na familia hii ni mojawapo ya chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani na hata mauaji ya kutisha tunayoyaona katika jamii na kundi kubwa la waathirika ni wanawake na watoto, pia zipo tabia na desturi kandamizi tuendelee kuelimisha kanisa ili waumi wetu wawe mstari wa mbele katika mabadiliko haya”.amesema Askofu Bugota.
Askofu Bugota ametumia nafasi hiyo kuwaomba
wanawake hao kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo zile za kiuchumi
ili kupata vyanzo vya mapato vitakavyowawezesha kujikwamua kimaisha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa idara ya wanawake kanisa la AICT Martha Misoji amemshukuru Askofu Bugota ambapo ameahidi kuwa idara hiyo itaendelea na jitihada mbalimbali za kuwaimarisha wanawake wa kanisa hili.
Amesema Dayosisi zinazoshiriki semina hiyo ni
Dayosisi ya Pwani, Dayosisi ya Mwanza, Dayosisi ya Geita, Mara, ukelewe pamoja
na Dayosisi ya kati.
Naye Mwenyekiti wa CCT Naila Mayala ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa mabalozi wazuri
kwa wengine.
Aidha Naila amewaomba wanawake hao
kuendelea kushirikiana katika kutokomeza Mmomonyoko wa maadili na kutoa elimu
juu ya malezi na makuzi ya watoto.
Wanawake wa kanisa la AICT katika Dayosisi
saba leo Jumatano Juni 14,2023 wameanza semina ya siku tatu yenye lengo la
kuwaimarisha kimwili na kiroho kukemea mambo maovu ikiwa ni maandalizi ya
kuelekea wiki ya wanawake inayofanyika kila Mwaka mwezi Septemba.
Social Plugin