Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGODI WA BARRICK BULYANHULU WABORESHA HUDUMA ZA MATIBABU HOSPITALI YA WILAYA YA NYANG'HWALE

 

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu waboresha huduma za matibabu Hospitali ya wilaya ya Nyang’hwale

Na Marco Maduhu, GEITA

MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita Husna Toni, amesema Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo kwenye Halmashauri hiyo, ikiwamo na uboreshaji wa huduma za matibabu katika Hospitali ya wilaya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale Husna Toni.

Amebainisha hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambao walitembelea Halmashauri hiyo kuona miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetekelezwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia fedha za CSR.
Jengo la wodi la wagonjwa dharura katika Hospitali ya wilaya ya Nyang'hwale.

Amesema wilaya hiyo ya Nyang’hwale ni mpya, lakini wanaushukuru Mgodi huo kwa kushirikiana vyema na Serikali katika kuchochea maendeleo, na kutekeleza miradi mingi ikiwamo ya sekta ya Afya.
Jengo la wodi la wagonjwa dharura katika Hospitali ya wilaya ya Nyang'hwale.

“Katika Hospitali yetu ya wilaya hapa Nyang’hwale Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umetujengea wodi ya wagonjwa binafsi, na na kutuunga mkono kumalizia wodi ya wagonjwa wa dharura, pia umejenga na Zahanati 10 na ukamilishaji wa Maboma yaliyoanzishwa na nguvu za wananchi”amesema Toni.
Jengo la wodi la wagonjwa binafsi katika Hospitali ya wilaya ya Nyang'hwale.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya wilaya ya Nyang’hwale Dk. Princepius Mugishagwe, amesema wodi hizo mbili ni muhimu sana katika uboreshaji wa utoaji wa huduma za matibabu kwa wananchi na kuokoa Afya zao.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya wilaya ya Nyang’hwale Dk. Princepius Mugishagwe.

Nao baadhi ya Wananchi wa Nyang’hwale akiwamo Agostine Ramadhani, wamesema uboreshaji wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo ya wilaya, umewaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu zaidi kilomita 87 kwenda katika Hospitali ya Mkoa Geita kupata matibabu.
Mwananchi Agostine Ramadhani.

Kaimu Meneja Mahusiano ya Jamii kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo, amesema katika ujenzi wa jengo la wodi ya wagonjwa wa dharura wameshirikiana na Serikali kukamilisha ujenzi huo na kutoa Sh.milioni 69, huku wodi ya wagonjwa binafsi wamejenga wenyewe kwa zaidi ya Sh,milioni 100.
Kaimu Meneja Mahusiano ya Jamii kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Zuwena Senkondo.
Baadhi ya Vifaa Tiba vikiwa ndani ya Jengo la Wodi la Wagonjwa dharura katika Hospitali ya wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com