Na Mwandishi wetu
Mahakama ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida imetoa amri ya zuio la muda kwa kwa kikundi cha Vijana Victory Farmers kusafirisha Mbolea ya Samadi iliyokusanywa kutoka kwa wafugaji katika kijiji cha Ngaiti wilayani Manyoni.
Zuio hilo ni kutokana na kesi ndogo iliyofunguliwa kwa hati ya dharura na kampuni ya Maisha Transport limited baada ya kikundi hicho kukiuka mkataba baina yao
Kesi ya maombi madogo namba 3 ya mwaka 2023 ya kuzuia usafirishaji wa Mbolea hiyo baada ya ukiukwaji wa mkataba kwa kuuza mbolea hiyo kwa kampuni nyingine.
Kikundi hicho kiliingia mkataba wa mwaka 1 mwezi Januari 2023 na kampuni ya Maisha kwa kuuziana mbolea ya Samadi ambayo ilikusanywa kwenye kijiji cha Ngaiti wilayani Manyoni kutoka kwa wafugaji kwa makubaliana ya malipo ya shilingi milioni 30 kwa trip 79 za Semi trela.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Manyoni, Alisile Mwankejela amesema uamuzi huo umefuatia kufunguliwa kesi ya maombi madogo namba 3 ya 2023 kwa hati ya dharura juu ya usafirishwaji wa Mbolea hiyo.
Wakili wa upande wa madai John Chigongo amesema amepoka maamuzi hayo kwa moyo mkunjufu kwani yamewanusuru wateja wake kupata hasara wakati wakisubiri maamuzi ya kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2023.
Kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2023 inatarajia kusikilizwa tarehe 30.6.2023 katika Mahakam ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Social Plugin