Manispaa ya Shinyanga yaadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga, imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika, huku Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiwataka wazazi watumie Teknolojia kwa maendeleo endelevu na siyo kusababisha Mmomonyoko wa Maadili.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Maadhimisho hayo ya siku ya Mtoto wa Afrika katika Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Juni 15, 2023 katika Viwanja vya Sabasaba, ambapo kilele chake Kitaifa na Mkoa wa Shinyanga kitafanyika kesho Juni 16.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Samizi akizungumza kwenye Maadhimisho hayo, amewataka wazazi katika ulimwengu huu wa kidigital watumie Teknolojia kwa maendeleo endelevu na siyo kusahau malezi bora ya watoto kuwa bize na mitandao, na hatimaye kusababisha Mmomonyoko wa Maadili.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
“Ulimwengu huu wa digital unafursa mbalimbali endapo ukitumika vizuri kwa maendeleo endelevu, lakini ukitumika vibaya ndiyo chanzo kikuu cha Mmomonyoko wa maadili kwa watoto,”amesema Johari.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi.
Aidha, amewataka pia wazazi wasiruhusu watoto wao wakuchezea simu za wakubwa, huku akiwasihi pia wawe makini na maudhui ya ‘Cartoon’ ambazo wana angalia watoto ili kutoiga mambo ya ajabu ambayo ni kinyume na maadili ya Mwafrika.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya, amewataka watoto wasikubali kushikwa shikwa katika maungo yao, na mtu ambaye akiwafanyia vitendo hivyo watoe taarifa kwa Walimu, Wazazi, Maofisa Maendeleo, Ustawi au kwa kiongozi yoyote wa Serikali ili achukuliwe hatua.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amesema Serikali itaendelea kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili, pamoja na kuunda Mabaraza ya watoto ambayo husaidia kupasa sauti za vitendo vya ukatili.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga Grace Ngowi akisoma taarifa ya watoto kwenye Maadhimisho hayo, amewaomba viongozi wa Serikali kuendelea kuwajibika ipasavyo juu ya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wadogo, pamoja na kuharakisha utolewaji wa hukumu kwa watu ambao wameshitakiwa kufanya vitendo hivyo.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga Grace Ngowi .
Kauli Mbiu ya mwaka huu ya Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika inasema ‘zingatia usalama wa watoto katika ulimwengu wa kidigital.’
Tazama picha hapa chini maadhimisho siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga👇👇
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Maadhimisho siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga yakiendelea.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiangalia vipaji vya watoto ambavyo hufundishwa mafunzo ya ufundi kupitia Commpasion.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiangalia Chandarua ambacho kimetengenezwa na watoto.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akiangalia bidhaa mbalimbali ambazo zimetengenezwa na watoto.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko wakiangalia bidhaa za viatu ambavyo vimetenegezwa na watoto.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kushoto) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko wakiangalia bidhaa za viatu ambavyo vimetenegezwa na watoto.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kulia)akipokea picha yake ambayo imechora wa vijana wa Commpasion kutoka Kanisa la AICT Kitangili.
Mwonekano wa Picha ya DC Johari Samizi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kulia)akipokea picha yake ambayo imechora wa vijana wa Commpasion kutoka Kanisa la AICT Kitangili.
Awali watoto wakiwa kwenye maandamano katika maandisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa kwenye maandamano katika maandisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakionyesha Mabango yenye ujumbe katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakionyesha Mabango yenye ujumbe katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (katikati) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kulia) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii John Tesha, wakipokea Maandamano.
Watoto wakiwa na Bango lenye ujumbe katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Shinyanga.
Social Plugin