Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKANDARASI kutoka Kampuni ya Sinohydro Corporation ya nchini China, ametambulishwa rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa umeme wa Jua wilayani Kishapu kwa awamu ya kwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Meneja Mradi wa umeme wa Jua kutoka TANESCO Makao Makuu Dodoma Mhandisi Emmanuel Anderson, akizungumza wakati wa utambulisho wa Mkandarasi huyo, amesema mradi wa umeme wa Jua wilayani Kishapu ni wa Megawatts 150, na utakuwa ukitekelezwa kwa awamu awamu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo.
Amesema Mkandarasi huyo kutoka Kampuni ya Sinohydro Corporation ya Nchini China, atatekeleza ujenzi wa umeme huo wa Jua wilayani Kishapu kwa awamu ya kwanza Megawatts 50.
“Leo tumekuja hapa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kumtambulisha Rasmi Mkandarasi ambaye atatekeleza ujenzi wa mradi wa umeme wa Jua awamu ya kwanza Megawatts 50, na Mkataba wake wa ujenzi utaisha Agosti mwakani (2024),”amesema Mhandisi Emmanuel.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amempongeza Rais Samia kwa mradi huo mkubwa wa umeme wa Jua kuupeleka wilayani Kishapu, na kumwahidi Mkandarasi huyo kwamba Serikali itakuwa naye bega kwa bega kwa hatua zote za utekelezaji wa mradi huo, na kumtaka aukamilishe ndani ya muda wa Mkataba.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya Mkandarasi wa utekelezaji wa mradi umeme wa Jua wilayani Kishapu kutambulishwa Rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Social Plugin