Wabunge wakitoka Bungeni - Picha na MWANANCHI
Katika hali isiyotarajiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirisha kwa muda kikao chake wakati wabunge wakiendelea kwenye kipindi cha maswali na majibu baada ya king'ora kinachoashiria kuna jambo la hatari kulia ndani ya ukumbi wa Bunge.
Kufuatia kupiga kelele kwa king'ora bungeni majira ya saa 3:50 leo asubuhi leo Jumanne Juni 27, 2023 ndipo Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akaahirisha shughuli za Bunge.
"Waheshimiwa wabunge hiyo sauti inaashiria tutoke humu ndani kwa haraka sana, kila mmoja atafute mlango wa kutoka na sote twendeni lile eneo la kukusanyikia, naahirisha shughuli za Bunge hadi hali itakapotulia", amesema Dkt. Tulia.
Social Plugin