Katibu Valentine Maganga (kushoto) akipokea zawadi ya pea ya shuka za kisasa kutoka kwa CEO Jacob Mugini.
CEO Mugini (kulia) akimkabidhi Katibu wa Wazazi CCM Wilaya ya Tarime, Mathias Lugola zawadi ya pea ya shuka za kisasa kwa ajili ya Katibu wa Wilaya, Noverty Batholomeo ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake.
ALIYEKUWA Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, Valentine Maganga - aliyehamishiwa Wilaya ya Musoma (Vijijini), ameagwa rasmi katika hafla iliyofana kwa aina yake, ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkurugenzi na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara, Jacob Mugini.
Hafla hiyo ambayo iliandaliwa na Shirikisho la Walimu Makada wa CCM, ilifanyika katika ukumbi wa Goldland Hotel mjini Tarime, jana Jumapili.
“Nimefurahi kushiriki katika hafla hii, mimi sina chama lakini nina marafiki wengi CCM na naipenda CCM kwa mambo mazuri inayofanya katika kuliletea taifa letu maendeleo,” alisema Mugini ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mara Online.
Mbali na kuwapa Katibu Maganga na Katibu mpya wa CCM Wilaya ya Tarime, Noverty Batholomeo zawadi ya pea za shuka za kisasa, Mugini alisema ofisi yake imekuwa ikifuharia kufanya na watendaji wa chama hicho katika ngazi mbalimbali.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Tarime, Marema Solo ndiye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wilaya wa chama hicho, Daudi Marwa Ngicho.
Wageni wengine walioshiriki katika hafla hiyo ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chonchorio ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara, na Diwani wa Kata ya Nyanungu, Tiboche Richard.
Chonchorio ambaye ni kada kijana wa chama hicho tawala na mfanyabiashara; naye alikabidhi zawadi yake kwa Katibu Maganga kama ilivyokuwa kwa wengeni wengine mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Chonchorio pia alishusha tabasamu zaidi kwa makada hao walimu wa CCM, baada ya kuwachangia shilingi milioni moja ili kuwawezesha kuanzisha mradi wa kujiingizia kipato.
Chonchorio amewaka historia ya kuwa kiongozi wa CCM wa kwanza kusaidia maendeleo ya walimu hao.
Awali, walimu hao kupitia risala yao walisema moja ya changamoto waliyonayo ni kupata mradi wa kujipatia kipato kwa maendeleo ya umoja wao.
CHANZO- SAUTI YA MARA
Social Plugin