MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameishukuru serikali kwa kuanza kutekeleza mradi wa maji katika Vijiji vya Minyinga,Mkunguwakihedo na Sakaa vilivyopo wilayani Ikungi Mkoani Singida ambapo kukamilika kwake kutaleta faida kubwa kwa wananchi.
Pamoja na shukrani hizo ameihoji serikali ni lini italipa fedha ili mkandarasi anayejenga miradi ya maji katika vijiji hivyo amalizie kazi aliyoianza kuitekeleza.
Akiuliza swali Juni 6,2023,Bungeni Jijini Dodoma Mtaturu amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutaleta faida kwa vijiji hivyo.
“Tunaishukuru sana serikali kwa kuanza kutekeleza mradi wa maji katika vijiji vya Minyinga,Mkunguwakihendo na Sakaa ,lakini kwa masikitikko makubwa mh mwenyekiti mpaka sasa miradi imesimama na inasemekana mkandarasi hajalipwa,je ni lini serikali italipa fedha ili mkandarasi amalizie miradi ile ambayo ina faida kubwa kwa wananchi,”amehoji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Marryprisca Mahundi amesema ni kwlei miradi inaendelea na kama wizara wameshaanza kulipa wakandarasi.
“Hapo katikati fedha hatukuwa nayo lakini tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ametupatia fedha tayari na tunaanza kulipa wakandarasi,”amesema.
Social Plugin