Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Mussa Misaile akifunga mafunzo kwa Wajumbe wa Bodi wa vyama vipya vya Ushirika wa Mbogamboga, matunda na mazao mchanganyiko, Mkoani Arusha
Wajumbe wa Bodi za Vyama vipya vya Ushirika wa Mbogamboga, matunda na mazao mchanganyiko wakifuatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Arusha Mussa Misaile baada ya mafunzo ya Ushirika
Na.Mwandishi Wetu
Wanachama wa Chama cha Ushirika wametajwa kuwa wamiliki wa kwanza wa Chama cha Ushirika. Hivyo, wana wajibu wa kulinda na kusimamia Chama cha Ushirika kuendeshwa kwa tija kwa maslahi ya Wanachama wa Chama cha Ushirika.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Mussa Misaile akifunga mafunzo yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi wa Vyama vipya vya Ushirika kutoka Halmashauri za Wilaya za Karatu, Meru na Arusha wanaolima mazao ya Mbogamboga, matunda na mazao mchanganyiko yaliyoanza Juni 5, 2023 na kuhitimishwa Juni 7, 2023 Mkoani Arusha.
Katibu Tawala amewaasa Viongozi kwenda kusimamia na kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha kwamba wanasimamia wanachama wao kutimiza wajibu wao ikiwemo ulipaji wa hisa utakao changia katika kujenga na kuimarisha mtaji wa Chama, kulipa viingilio, kushiriki wa Mikutano mikuu, Chaguzi za Vyama pamoja na majukumu mengine yaliyowekwa kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya Chama.
Social Plugin