KANISA LA IEAGT SHINYANGA LIMEADHIMISHA WIKI YA WATOTO, ASKOFU MABUSHI ALIA MAUDHUI YA TAMTHILIA ZA MAPENZI KUHARIBU MAADILI YA WATOTO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KANISA la International Evangelical Assemblies Of God Tanzania( IEAGT) Kambi ya Waebrania Manispaa ya Shinyanga, limeadhimisha wiki ya watoto na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali.
Askofu Mabushi akiwa na Mkewake.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Juni 25,2023 Kanisa hapo, na kuonyeshwa vipaji vya kuhubiri, kukariri Mafungu ya Biblia, kuimba nyimbo, Ngojera na Maigizo yaliyo na mafundisho ya neno la Mungu.
Wazee wa Kanisa la IEAGT.

Akitoa neno la Mahubiri Mtoto Ebenezer Ezekiel lisemalo kuishi maisha matakatifu, ameitaka jamii ili kuishi maisha hayo ni kuacha kutenda dhambi, pamoja na watoto wasisikilize ushauri mbaya kutoka kwa marafiki na kuingia katika matendo mabaya.
Mtoto Ebenezer Ezekiel akitoa Mahubiri

Naye Mtoto Vanesa Ephata akisoma hotuba kwa niaba ya wenzake, amewaomba wazazi wazingatie malezi bora ya watoto wao na kuacha kuwa bize na mitandao ya simu na kuathiriwa na ulimwengu wa kidigital na kusababisha Mmomonyoko wa maadili kwa watoto.
Mtoto Vanesa Ephata akisoma hotuba.

"Leo tunahitimisha wiki ya watoto hapa Kanisani na ujumbe wetu kwa wazazi wazingatie usalama wa watoto katika ulimwengu huu wa kidigital, na waache kufanya vitendo vya ukatili kwa watoto," amesema Vanesa.
Aidha, amewaomba wazazi wapendane na kuacha kurumbana mbele ya watoto pamoja na kutoleana lugha chafu, huku wakiiomba Serikali nyimbo zenye maudhui mabaya kwa watoto zipigwe marufuku.
Askofu wa Kanisa hilo la IEAGT David Mabushi akitoa neno amewataka wazazi katika ulimwengu huu wa kidigitali wawe makini na malezi ya watoto wao, pamoja na kudhuia kuangalia Tamthilia zenye maudhui ya kimapenzi ambazo zimekuwa chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa maadili ya watoto.
Askofu David Mabushi

Ametoa wito pia kwa watoto wasipende kuiga mambo mabaya ambayo yatapoteza dira ya maisha yao, bali waendelee kumcha Mwenyezi Mungu na kuhudhuria mafundisho ya neno la Mungu Kanisani.

Tanzama picha mbalimbali maadhimisho wiki ya watoto kanisa la IEAGT.👇👇
Mtoto Ibrahimu Jacob akitoa Matangazo ya Kanisa kama Mzee wa Kanisa kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya watoto.
Mtoto Ebenezer Ezekiel akitoa Mahubiri huku akisoma Mafungu ya neno la Mungu katika Biblia.
Mwalimu wa watoto Kanisa la IEAGT Rehema Mpongo akitoa neno kwenye Maadhimisho ya wiki ya watoto Kanisani hapo.
Watoto wa Kanisa la IEAGT wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya watoto Kanisani hapo.
Maadhimisho ya wiki ya watoto Kanisa la IEAGT yakiendelea.
Watoto wakionyesha vipaji vya kukariri Mafungu ya kwenye Biblia.
Watoto wakisoma neno la Mungu kwenye Biblia kwa kufuatisha wenzao wanavyokariri Mafungu ya Biblia.
Watoto wakiendelea kuonyesha vipaji vya kukariri Mafungu ya kwenye Biblia.

Watoto wakionyesha vipaji vya kuimba nyimbo za neno la Mungu.
Watoto wakiendelea kuonyesha vipaji vya kuimba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post