Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Shinyanga.
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
KIONGOZI wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameeleza kusikitishwa na Mikoa yenye utajiri wa Rasilimali nyingi ikiwamo ya Madini kukabiliwa na wimbi kubwa la umaskini.
Amebainisha hayo leo Juni 6,2023 kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Zimamoto Manispaa ya Shinyanga.
Amesema Mikoa ya Kanda ya Magharibi na Kanda ya Ziwa, ina utajiri mkubwa wa Rasilimali lakini Mikoa hiyo ipo nyuma kimaendelo pamoja na kukabiliwa na umaskini mkubwa.
"Umaskini katika Mikoa hii yenye utajiri wa Rasilimali nyingi unasababishwa na Sera mbovu za viongozi wetu kutoka Chama Cha Mapinduzi ambazo hazina ushindani, hivyo tunataka mabadilko makubwa na kuiondoa CCM," amesema Zitto.
"Sisi ACT-Wazalendo tukipata ridhaa ya kuongoza nchi, Sera yetu ni Taifa la wote Maslahi ya wote, ili Watanzania tunufaike wote na utajiri wa Rasilimali za nchi yetu na siyo watu wachache," ameongeza.
Aidha, amesisitiza pia suala la Mabadiliko ya Katiba Mpya, ambayo ndiyo itakuwa mkombozi mkubwa kwa Watanzania na kuwaondoa kwenye dimbwi la umaskini na kuwaletea Maendeleo, pamoja na kuwapo wa sheria mpya ya uchaguzi ili kuanzisha Tume huru ya uchaguzi.
Katika hatua nyingine amekemea tatizo la utolewaji wa Bima za Afya kwa Matabaka, na kutaka Bima hizo zitolewe sawa kwa watu wote na siyo kubaguana na kuumiza watu wenye kipato cha chini kwa kukosa huduma bora za matibabu
Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Doroth Semu, akizungumza kwenye Mkutano huo ameisisitiza Serikali kutoa Pesheni bora kwa Wastaafu.
Naye Naibu Msemaji wa Sekta ya Elimu kutoka Chama Cha ACT-Wazalendo Bahati Chirwa, akizungumza kwenye Mkutano huo, ameiomba Serikali kuongeza Ruzuku kwenye utolewaji wa fedha za elimu bure,ili kuondoa utitiri wa michango mashuleni ambayo inaondoa maana ya elimu bure.
Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Siri Yasini, amewaomba Watanzania kukiunga Mkono Chama hicho hasa katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani, na kuchagua viongozi watokanao na chama hicho ambao ndiyo watapigania maslahi yao na kuwaletea maendeleo.
Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Shinyanga.
Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo Doroth Semu akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Shinyanga huku akiendelea kunyeshewa na mvua.
Waziri Kivuli wa Elimu kutoka Chama Cha ACT-Wazalendo Bahati Chirwa akizungumza na Wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
Waziri Kivuli wa Fedha kutoka Chama Cha ACT-Wazalendo Emmanuel Mvula akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Shinyanga.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chama Cha ACT-Wazalendo Msafiri Mtemelwa akizunguma na Wananchi wa Shinyanga kwenye Mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoani Shinyanga Siri Yasini akizunguma kwenye Mkutano huo wa hadhara.
Viongozi wa ACT-Wazalendo wakiwa meza kuu
Viongozi wa ACT-Wazalendo wakiwa meza kuu.
Viongozi wa ACT-Wazalendo wakiwa meza kuu
Viongozi wa Chama Cha NRA wakiwa kwenye Mkutano wa ACT-Wazalendo.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa ACT-Wazalendo.

Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa ACT-Wazalendo licha ya kunyeshewa na mvua waliendelea kusikiliza sera za viongozi mbalimbali wa Chama hicho.
Wananchi wakiendelea kunyeshewa na mvua huku wakijifunika viti na kuendelea kusikiliza sera za Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa ACT-Wazalendo.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa ACT-Wazalendo.
Social Plugin