Na Dotto Kwilasa, Dodoma.
Hatimaye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha azimio la kuridhia Mkataba baina ya Serikali ya
Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World kuhusu
Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania.
Hatua hii ni baada ya kupokea mapendekezo ya Wawekezaji mbalimbali wakiwemo kampuni ya Hutchson(Hong Kong), Antewerp/Brugge(Belgium), PSA International (Singapore), DP World(Dubai), Abu Dhabi Ports(AbuDhabi), Adani
Ports and Logistics(Mundra-India), Kampuni ya CMA-CGM(France) pamoja na Kampuni ya Maersk(Denmark).
Hayo yamejiri leo June 10,2023 Jijini hapa ambapo mkataba huo unatajwa kuleta manufaa katika kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 mpaka masaa 24 na kupunguza gharama za utumiaji wa Bandari na kufungua masoko ya kimkakati katika eneo la bidhaa na biashara ya usafirishaji ndani ya nchi na kanda jirani.
Akitoa maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya mkataba huo
Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mnyaa Mbarawa Mheshimiwa Spika,katika kupitia mawasilisho ya kampuni hizo pamoja na sifa zao kimataifa, Serikali iliamua kuanzisha majadiliano na kampuni ya DP World kwa kuzingatia uzoefu wake katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini.
Ameeleza kuwa Kampuni hiyo ina uzoefu na utaalamu
wa kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka maeneo ambayo bidhaa zinatoka mpaka kufika kwa Walaji na kueleza
ameeleza kuwa uwekezaji huo utaongeza idadi ya meli zitakazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569
zilizohudumiwa mwaka 2021/22 mpaka kufikia takriban meli
2,950 ifikapo mwaka 2032/33.
Hata hivyo Waziri huyo amebainisha kuwa muda wa ukomo wa mkataba utakaosainiwa haujawekwa wazi na badala yake Serikali imewaachia suala hilo wataalamu wa sheria za Uwekezaji.
"Tutaweka muda ukomo na muundo wa marejeo Kwa kupitia viashiria muhimu vya kiutendaji na ikiwa mwekezaji yeyote atashindwa kutekeleza majukumu yake tunaachana nae , hatuwezi kuwavumilia watu wasio na uwezo,"Amesema Waziri huyo.
Aidha ameeleza kuwa muda wa ushushaji wa makontena utapungua kutoka siku 4.5 mpaka siku 2 ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12
mpaka saa 1 kutokana na uboreshaji wamifumoya TEHAMA.
"Uwekezaji huu unatarajiwa kupunguza gharama ya usafirishaji wa mizigo kutoka nchi za nje kwenda nchi za Jirani, kwa mfano kutoka US$12,000 mpaka kati ya US$6,000 na US$7,000kwa kasha linalokwenda nchi ya Malawi, Zambia au DRC na kuleta watumiaji wengi kwenye Bandari ya Dar es Salaam,"amesema
Waziri huyo ametaja manufaa mengine kuwa ni kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni
18.41 za mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka
2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 158 na kuongezeka kwa mapato ya Serikali yatokanayo na kodi ya forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa
bandarini kutoka Shilingi Trilioni 7.76za mwaka 2021/22 hadi
Shilingi Trilioni 26.7za mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la
asilimia 244.
"Uwekezaji huu mkubwa utasaidia kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 mwaka 2021/22 hadi ajira71,907 ifikapo mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 148,maboresho ya maeneo ya kuhudumia shehena ya makasha na kuweka mitambo yenye Teknolojia ya kisasa,"amefafanua
Manufaa mengine ni kuendeleza eneo la kuhifadhia mizigo la Bandari Kavukwa kuweka miundombinu ya kisasa ya kuhudumia aina zote za shehena,maboresho ya magati ya kuhudumia majahazi na abiria ikiwa ni pamoja na kushawishi uingiaji wa meli kubwa za kitalii zitakazo ongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la
Taifa.
"Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika
Bandari zote uanzishwaji wa maeneo Maalum ya Kiuchumi/Viwanda,kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, kuchagiza shughuli za Viwanda na Biashara, kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za usafirishaji kwa njia ya reli,"amesema
Prof.Mbalawa ameeleza kuwa kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam kulisababisha meli kusubiri muda mrefu nangani ambako kunasababishakuongezeka kwa gharama ya kutumia bandari ya Dar es Salaam, kwa mfano gharama za meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takriban Dola za Marekani 25,000, sawa na takriban
Shilingi milioni 58kwa siku.
Pia kunaongeza gharama katika mnyororo mzima wa usafirishaji (total route costs)kutoka njeya nchi, kupitia katika bandari kwenda nchi za jirani zinazotumia bandari na kutolea mfano, gharama ya kusafirisha kasha moja kutoka nje ya nchi(ontransit)kwenda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo (DRC) zinafikia takriban Dola za Marekani kati ya 8,500 hadi 12,000.
" Hii ni gharama kubwa sana ikilinganishwa na Bandari shindani,kwa kutambua kuwa Serikali pekee haitaweza
kutatua changamoto zilizopo kwenye Bandariya Dar es salaam,
kuanzia miaka ya 2000, Serikali ya Awamu ya Tatu kupitia Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) iliingia mkataba wa upangaji na uendeshaji na
Kampuni ya Kimataifa ya Uendeshaji wa Vitengo vya Makasha,
Hutchison ya Hong-Kong China. Mkataba huo ulidumu kwa miaka Minne,"amesema
Ili kutoa fursa kwa Wawekezaji wengine
kuwekeza katika maeneo mengine ya bandari nchini kwa lengo la kuleta ushindani, tija na ufanisi,Waziri huyo ameeleza kuwa uwekezaji tarajiwa chini ya Mkataba huu hautahusisha maeneo ya Gati namba 8 hadi 11, Gati la Mafuta Kurasini Na. 1,Gati la Mafuta Kurasini Na. 2 ,Boya la Kupokelea Mafuta na Gati la
Kuhudumia Magari katika Bandari ya Dar es Salaam na
maeneo yote ya Awamu ya Kwanza na Pili ambayo hayatafikia
muafaka katika majadiliano yatakayofanyika baada yakuridhiwa kwa IGA.
Alisema Uwekezaji huo pia, hautahusisha Bandari ya Tanga na Mtwara na kwamba mkataba huo unatoa haki ya upekee ya kufanya majadiliano kwa Awamu ya Miradi iliyoanishwa kwenye Mkataba huo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili.
" Msingi wa kutoa haki hii ya kipekee ni kuwezesha pande mbili kufanya majadiliano na kumpa uhakika Mwekezaji kujadiliana katika maeneo pasipo kuwepo
kwa majadiliano na Mwekezaji mwingine katika maeneo hayohayo,iwapo kipindi hicho kitakwisha bila kufikia makubaliano, TPA inaweza kuanzisha majadiliano na Wawekezaji wengine katika maeneo hayo pasipo kuwepo kwa mgogoro wowote chini ya Mkataba
huo,"ameeleza.
Kuhusu muda wa uhai wa Mkataba huo, amesema utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na mikataba ya miradi .
Prof.Mbarawa amebainisha kuwa mkataba huo utazingatia jukumu la Ulinzi na Usalama katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kusimamiwa na Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama ambavyo vipo katika maeneo yote ya Bandari kwa kuzingatia Sheria za nchi na mikataba ya kimataifa.
" Suala hili limezingatiwa pia katika Mkataba wa IGAna kuwekwa bayana kwamba masuala ya Ulinzi na Usalama hayatakiukwa kwa namna yeyote wakati wa utekelezaji
shughuli za uwekezaji, pia taasisi zote za Serikali ambazo
zinahusika katika shughuli za bandari zitaendelea kutekeleza
majukumu yao kwa mujibuSheria ndani ya eneo la bandari,"alisisitiza
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Seleman Kakoso ameeleza kuwa kati ya jambo la msingi
ambalo Kamati iizingatia katika uchambuzi wa uwekezaji huo, ni kutaka kufahamu na kujiridhisha kwamba Nchi
imeingia makubaliano ya aina gani na Serikali ya Dubai.
Kakoso alieleza kuwa baada ya kuihoji Serikali kuhusu suala hilo ili kujirdhisha kikamilifu,Kamati imebaini kwamba,
Makubaliano yaliyopo ni baina ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
Dubai juu ya kuweka msingi wa kisheria wa uendelezaji wa bandari.
"Aidha, aina ya ubia, kiasi/kiwango cha ubia, na maeneo ya
ubia yataainishwa kwenye Mikataba ya Utekelezaji itakayokuja kuingiwa baada ya Bunge kuridhia Azimio hili lengo Makubaliano Mheshimiwa Spika, katika uchambuzi wake, Kamati imebaini kwamba lengo ni kuweka msingiwa kisheria
katika maeneo ya ushirikiano ili kuendeleza na
kuboresha uendeshaji wa miundombinu,"alifafanua
Alitilia mkazo kuwa Kamati inasisitiza kwamba uhai wa mikataba ya Utekelezaji itakayosainiwa itaje muda
maalum wa utekelezaji wa miradi ambao utazingatia
maslahi mapana ya nchi.
Vilevile, mikataba hiyo iwe na kipengele kinachoelekeza wabia kufanya tathimini ya utekelezaji wa miradi ya uwekezaji,na kuvunja Makubaliano iwapo utekelezaji huo hautafanyika kama ilivyokusudiwa.
Kuhusu uhakika wa Ajira na Fursa kwa Watanzania Kakoso alieleza kuwa makubaliano yanayopendekezwa kuridhiwa na yana sura ya ubia na kwamba Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha kwamba ajira za Watanzania zinalindwa
na kuweka mfumo thabitiwa mgawanyo wa ajira
baina ya nchi wabia.