MILA na desturi za kiafrika zinachangia kwa kiasi kikubwa kuleta utofauti kati ya Mwanaume na Mwanamke kwenye ndoa hasa masuala ya uwajibikaji, mawasiliano pamoja na uwazi ambapo inapelekea kupata matatizo ya Afya ya akili.
Ameyasema hayo jana Juni 28,2023 Mwezeshaji wa Semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha kupunguza kasi ya kujiua Tanzania (TSPC), Bi.Matha Kalinga katika mdahalo kuhusiana na matatizo ya afya ya akili kwenye ndoa na familia.
Amesema wanaume ndo wanaongoza kwa kuwa matatizo ya afya ya akili kuliko wanawake kwneye ndoa ambalo tatizo hilo linapelekea kwa wanaume kutaka kujiua.
Aidha Bi.Matha ameiomba serikali kutengeneza mazingira rafiki kwa wale watu ambao wameathirika na afya ya akili ili waweze kupata msaada na kuondokana na tatizo hilo ambalo mara nyingi hupelekea kutaka kujiua.
"Ili kuondokana na tatizo hili la afya ya akili, unatakiwa kujihusisha na masuala ya michezo, kujichanganya na watu ili kuepuka kukaa peke yako". Amesema Bi.Matha.
Kwa upande wa washiriki wa mdahalo huo, wamepongeza uwepo wa mjadala huo kwani jamii imekuwa ikikumbwa na matatizo ya afya ya akili ambapo knapelekea famili nyingi kuathirika mpaka kwa watoto.
Social Plugin