Na Dotto Kwilasa, Dodoma.
MBUNGE wa Jimbo la Mvumi mkoani Dodoma, Livingstone Lusende amemjia juu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Freeman Mbowe kwa kitendo cha kudai Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa wameingia mkataba wa uendeshaji na uboreshaji bandari ya Dar es Salaam wakati yeye na Waziri wanatoka upande wa pili wa Muungano.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma Leo Juni 8,2023 Jijini Dodoma Lusinde amesema maneno hayo si ya kiungwana yanalenga kubomoa.
Hatua hii imekuja kufuatia Mbowe akiwa Italia, kuzungumza kuwa Rais anatoka Zanzibar na Waziri anatoka Zanzibar, bandari ya Dar es Salaam ni kuharibu Muungano kwanini ya Zanzibar haijahusika.
"Hayo siyo maneno ya kiungwana kutuaminisha kwamba ni kosa Rais kutoka Zanzibar ni makosa na Waziri kutoka Zanzibar huu ni ubaguzi,Mbowe amesema Rais Samia anatoka upande wa pili wa Muungano ni kitendo cha hovyo kuanza kuzalisha ubaguzi,” amesema.
Mbunge huyo pia amesema,"Ubaguzi wa Mbowe si wa kuuacha upite, tusiangalie kiongozi wa nchi anatoka wapi, tunafahamu uamuzi wa kuingia mkataba wa kuboresha bandari, unapingwa na wafanyabiashara ambao amekuwa wakinufaika na utendaji mbovu wa bandari wanaonufaika kwa kukwepa kodi,"anasisitiza.
Lusinde amesema, Mpango wa Serikali wa kuingia mkataba kuboresha bandari utalinda ajira na wafanyakazi waliopo kazini hawataondoka na kwamba hakuna mkataba wa miaka 100 kama ipo sehemu inayoonesha miaka wadhibitishe.
“Hivi Rais akitoka Kilimanajaro mipaka yake ni mlima tu, asizungumze kuhusu korosho za kusini au kuhusu zabibu azungumzie za Kilimanjaro tu,” anahoji na kuongeza,
“Kuwa mwenyekiti wa kudumu kuna hasara zake anaweza kuwa amechoka akili yake. Yeye ni mwenyekiti wa pili Chadema wakati CCM Rais Samia ni wa sita,” anasema.
Lusinde ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia kwa kufanya mambo mengi bila kujali anatoka upande gani wa muungano na kuwaomba watanzania wawe wasipotoshwe.
"Hoja zijibiwe kwa hoja,Mbowe anazungumza mambo yanayoleta athari kwa jamii. Hajui kama ni suala la bandari ni suala la Muungano,Rais kutolea uamuzi bandari au kuteuliwa Mzanzibar kuwa Waziri wa Fedha kama alivyokuwa Saada Mkuya ni jambo la kawaida,"amesema.
Social Plugin