Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LESENI ZA UMEME ZITAWAPA MAFUNDI THAMANI, UHAKIKA WA AJIRA


Mhandisi Mwandamizi wa umeme Kanda ya Kaskazini EWURA Mha. Tegemea Kamando, akifundisha wanafunzi wa VETA Tanga, kuhusu kanuni za ufungaji mifumo ya Umeme wakati wa semina ya EWURA kwa wanafunzi hao.
Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi na Huduma Tanga ( RVET-Tanga) wakifuatilia mada kuhusu umuhimu wa leseni za ufungaji mifumo ya umeme zinazotolewa na EWURA kwa mafundi umeme wote Tanzania Bara.
Wanafunzi wakisoma vipeperushi vyenye maudhui ya utaratibu wa kupata leseni za EWURA za ufungaji mifumo ya umeme wakati wa mafunzo yaliyofanyika chuo cha RVET-Tanga

Na Mwandishi Wetu

Mkufunzi wa Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi na Huduma (RVET)Tanga, Tantatiet Swai, ameeleza kwamba, leseni zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), kwa mafundi umeme, zitawapa uhakika wa ajira na kuongeza thamani ya kazi zao kwani watatambulika na kuaminika katika utekelezaji wa shughuli za ufungaji mifumo ya umeme.

Mkufunzi huyo ameeleza hayo , baada ya mafunzo ya utaratibu wa mafundi umeme kupata leseni za ufungaji mifumo ya umeme, yaliyotolewa na EWURA kwa wanafunzi 104, wanaosomea fani ya usanikishaji mifumo ya umeme majumbani, ngazi ya I na ya II katika chuo hicho.

Mha. Tegemea Kamando, amewaeleza wanafunzi hao kuwa, EWURA hutoa leseni kwa mujibu wa sheria, hivyo kuwa na leseni ni lazima na kinyume chake hupelekea adhabu ya faini isiyopungua milioni tano, kifungo jela au vyote kwa pamoja.

EWURA hutoa leseni kwa kuzingatia elimu na uzoefu wa mwombaji kwa ada ya shilingi 130,000 kwa leseni daraja A, B, S1, S2; huku daraja C,D, W na S3 ikiwa shilingi 50,000; ambazo hudumu kwa miaka mitano.

Maombi ya leseni hufanyika kieletroni kwa mfumo wa LOIS https://lois.ewura.go.tz/ewura/

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com