Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akipanda mti katika Bustani ya TASAF Ndembezi.
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama Chamapinduzi (CCM )Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amewataka wananchi kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zake.
Mabala amesema hayo leo Juni 25, 2023 katika viwanja vya bustani ya TASAF (zamani soko la Mirunda) Kata ya Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga wakati wa mkutano wa hadhara alio fanya katika kata hiyo ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha ziara yake ya siku saba aliyofanya kwa lengo la kuimarisha chama, na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi mkoani humo ya mwaka 2020 – 2025 ikiwa ni pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mabala amempongeza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuvuka lengo la bajeti sambamba na kusimamia vizuri matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Nampongeza Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya na sasa Mkoa wetu unang'aa kila mahali kutokana na fedha nyingi za maendeleo zilizo letwa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wamiradi mbalimbalimbali ikiwemo sekta ya Afya ,Maji,Nishati,Miundo mbinu na Elimu ,mesema Mabala.
Aidha Mabala amewataka wananchi wa Manispaa ya Shinyanga na mkoakwa ujumla kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi huku akiitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kuwa ni pamoja na Soko la kisasa, soko la mitumba na soko la wajasiriamali.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini Makombe akimkaribisha mwenyekiti wa CCM mkoa Mabala Mlolwa .
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akiongozana na Viongozi wa chama hicho wilaya na mkoa.
Wajumbe wa Chama cha Mapinduzi wilaya na mkoa wakiendelea na mkutano Ndembezi.
Burudani zikiendelea.
Burudani zinaendelea.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akimwagilia mti wake.
Katibu Chama Cha Mapinduzi kata ya Ndembezi akifanya utambulisho.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano
Wananchi wakiwa kwenye mkutano
Kaimu mtendaji wa kata ya Ndembezi akitoa taarifa ya kata.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akiwainua wataalamu kujibu kero za wananchi.
Wakuu waidara na vitendo wakisubiri kujibu hoja kwenye mkutano.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano
Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akijibu kero za wananchi kwenye mkutano
Social Plugin