Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHE.KATAMBI : MISHAHARA NA MASLAHI YA MADEREVA IMEBORESHWA




Na: Mwandishi Wetu, DODOMA

SERIKALI imesema mshahara na maslahi kwa madereva imeboreshwa kupitia amri ya kima cha chini cha mshahara kipya kilichoanza kutumika Januari mosi 2023.

Amesema, utaratibu wa kazi kwa madereva wanaoendesha magari ya IT unafanyika kwa kuingia makubaliano ya kazi kati ya mmiliki wa gari na dereva husika na malipo hufanyika baada ya mhusika kufikisha gari linapokwenda.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Mhe. Sophia Mwakagenda ambaye amehoji lini serikali itashughulikia kuboresha ujira wa madereva wa magari ya IT.

Mhe. Katambi akijibu swali lake, amesema serikali kwa kutambua mchango wa sekta mbalimbali katika uchumi ikiwamo sekta ya usafirishaji na tayari imepanga Kima cha Chini cha Mshahara kilichoboreshwa ambacho kimeanza kutumika Januari mosi, 2023.

Aidha, ametoa rai kwa madereva wa magari ya IT kuingia mikataba ya kazi ya kibiashara na pale na atatokea mwajiri au kampuni ambayo itaajiri madereva kwa ajili ya kuendesha magari ya IT atapaswa kuzingatia Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ambayo inaelekeza ulipaji wa ujira kulingana na sekta hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com