MTATURU ASHAURI KILIMO KIMUINUE MTANZANIA



Na Alex Sonna-DODOMA

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaruru ameipongeza serikali kwa kuongeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye bajeti ya Kilimo.

Pamoja na pongezi hizo ameiomba serikali kuangalia pendekezo lake la kupunguza ushuru wa forodha kwa mafuta ya kula yanayotoka nje ya nchi kutoka asilimia 35 mpaka 25 na kusema hatua hiyo itawavunja moyo wakulima .

Mtaturu ametoa ombi hilo Juni 21,2023,Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti Kuu ya serikali kwa mwaka 2023/2024.

“Tulikuwa tunalalamika nchi yetu ina upungufu wa mafuta ya kula mpaka tukalazimika kwenda kuagiza nje ya nchi,tumekuwa na fedha nyingi za kigeni tunatumia kwa ajili ya kununua mafuta nje ya nchi,ukaja mkakati kupitia wizara ya kilimo tuzalishe alizeti ya kutosha, tukaleta mbegu wananchi wakawezeshwa na hivi tunavyoongea wananchi wamevuna vya kutosha,sasa hivi bei ya debe ya alizeti imeshuka na wananchi wangu wanalalamika ,wanaomba serikali iwasaidie kuhakikisha kwamba ile alizeti yao iwape faida,

“Nimeangalia hapa namna ambavyo tunapunguza kodi kwenye mafuta yaliyosafishwa kutoka nje kwa asilimia 25 badala ya 35 iambayo tunadhani ingekuwepo ,niombe sana kwenye semi refined tunayo asilimia 10 lakini kwenye Crued Oil tunayo asilimia 0 ili kusaidia viwanda vya ndani,niombe sana kama tunataka kuendana na mpango mzuri wa Wizara ya Kilimo turudishe asilimia 35 kwenye refined ili isaidie kupunguza mazao yanayotoka nje kwa maana ya bidhaa ya nje isiingie ndani,”amesema .

Amesema hatua hiyo itasaidia kuwa na uwezo mkubwa wak uzalisha na kumsaidia mkulima aliyepo pale kijijini na kuleta maana kubwa kwa uwekezaji wa kilimo cha alizeti na kuongeza mafuta mazuri ya alizeti nchini.

“Kwa hiyo kwa maana ya kumkomboa mkulima na kwenda na lugha ya pamoja tunaomba sana mpandishe iwe kwa asilimia 35 badala ya 25 ambayo tunaipendekeza ambayo kiukweli itaenda kuua soko, itaenda kuua kilimo cha wananchi wetu wa kawaida ambao sio lengo la serikali ya Rais Samia,niombe sana Waziri unaporudi uje utuhakikishie hilo na wananchi wanasubiri huko nje wanatuambia tusaidieni, tuokoeni tuweze kupata faida ya kilimo chetu,ameeleza.

UNUNUZI WA NDEGE.

Katika suala la ununuzi wa ndege ya mizigo ambayo imepokelewa juzi na Mh Rais ,ameipongeza hatua hiyo kwak uwa inaenda kuongeza uwezo wa kuuza nje moja kwa moja mazao ya mbogamboga na yale ya matunda ikiwemo parachichi ambayo inatakiwa sana duniani.

“Kwenye eneo hili tumekuwa na mpango mzuri wa mazao ya Horticulture kwenye maeneo yetu,Wizara ya Kilimo ina mpango mzuri upande wa horticulture,lakini tumekuwa na changamoto ya vifaa vya kuhifadhia mbogamboga na matunda,tumekuwa na Cold Rooms kwa maana ya Truck ambazo zinasafirisha mazao yetu ili yasiharibike,lakini tumekuwa pia na Cold Room Equipments ambazo zinatakiwa katika maeneo ya mashamba ya wakulima wetu,niombe sana serikali uje na mpango wa kuondoa walau ushuru au kodi ili kuingiza vile vifaa ambavyo vinaenda kusaidia kilimo cha mbogamboga katika maeneo yetu,

“Hatua hiyi pia itasaidia ndege kupata mzigo mkubwa wa kupeleka nje ya nchi ili tuuze fedha za kigeni na kwak ufanya hivyo fedha za kigeni zitaingia nchini,niombe Mh Waziri ukiweza kufanya hivyo utasaidia kilimo cha wananchi wetu ambao wameamua kujiwekeza kwenye eneo hili lakini hii ndege tunayoinunua itakuwa na maana kubwa ya kuhakikisha tunasafirisha mzigo mkubwa kwenda nje ya nchi,”amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post