Na Oscar Assenga,TANGA
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga amesema wanamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kutoa sapoti ya kupanua wigo kwa wanachama wao.
Hayo yalisema leo na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Audrey Claudius wakati wa maonyesho ya 10 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Alisema baada ya Serikali kuona wananchi wengi wanafanya biashara lakini hawana mfuko rasmi wa kuweka mafao na kutunza fedha zao kwa ajili ya matumizi ya baadae hivyo waliona waanzisha mfumo mpya wa Niss.
Aidha alisema kupitia mfumo huo wanachama wanaweza kujitunzia akiba zao kila mwezi na hivyo kuwa na sifa ya kupata mafao yao baadae lakini ili waweze kuwa mwanachama wa National Informal Sector Scheme (NISS) lazima waandikishwe wapate namba ya uanachama.
Meneja huyo alisema kwamba wakishapata namba ya uanachama naa akishaanza kuchanga kila mwezi kuna mafao wanayotoa kama mafao ya mateniti kwa wakina mama na mafao ya uzee baada kila kazi kuna mwisho wa ajira.
Hata hivyo alisema kwamba wameendelea kuboresha huduma zao na hivyo kuwezesha waajiri kuweza kufanya malipo ya michango ya wafanyakazi wao wakiwa ofisini au majumbani.
Alisema kwa sababu wanaweza kulipa kupitia mifumo ya kieletroniki ikiwa na Portal kufanya malipo kwa wafanyakazi wako pia mwanachama anaweza kuangalia salio lake akiwa nyumbani kwa kutumia simu yake ya mkononi.
“Sio hivyo tu wale waliofungua madai anaweza kuangalia mchakato wa faili lake limefikia wapi”Alisema
Hata hivyo Meneja huyo alisema kwamba wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo ya ili kutoa elimu inayohusiana na hifadhi ya jamii na kutoa huduma kwa wanachama wao.
Alisema kwamba wanatoa elimu kwa wafanyakazi walioajiriwa na waliojiajiri wenyewe kutokana na kwamba mfuko huo wameanzisha huduma kwa wanachama ambao wanajiingizia kipato wao.
Social Plugin