Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Juni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 3,2023
**************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI inatarajia kupokea ndege ya kwanza ya kusafirisha mizigo aina ya Boeing 767 -300 mnamo tarehe tatu Juni itakayokwenda kutatua changamoto za usafirishaji wa mizigo kwa wafanyabiashara nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 1,2023 Jijini Dar es Salaam, Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kukosekana kwa ndege ya mizigo toka nchini kwenda nchi za nje kumechangia ucheleweshwaji wa bidhaa pamoja na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji.
"Zaidi ya Tani elfu 24 za bidhaa ya samaki, mbogamboga na maua toka nchini zimekuwa zikisafirishwa kupitia mashirika mengine hivyo ujio wa ndege hii utatoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kutekeleza majukumu yao kwa urahisi". Amesema Prof.Mbarawa
Aidha amesema tukio hilo la kupokea ndege litafanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi ambaye ataongoza kupokea ndege hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Nae Afisa uhusiano wa Shirika la Ndege Tanzania Bi.Sarah Ruben amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji nchini kuwa ndege hiyo itakuwa na ratiba maalum itakayotoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuweza kuitumia. Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Juni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 3,2023
Social Plugin