Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba wakimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tatu (3,000,000/=) Mwalimu Sophia Mosses Kawegere wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ambaye ameibuka mshindi wa kwanza katika shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika Jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam.
****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Wizara ya wa Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza utaratibu mpya katika ajira za taaluma ya ualimu ambapo ili uajiriwe kuwa mwalimu utapaswa kufanya mtihani wa kupima uwezo wako.
Utaratibu huo umetolewa jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa walimu walioshinda shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati, lililoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Prof.Mkenda amesema kwa sasa, ajira ya ualimu inahusisha kutuma maombi katika tovuti maalum ya maombi ya ajira, kisha anayepata nafasi hufanyiwa usaili kisha kupangiwa eneo la kazi ivyo basi utaratibu huu utaanza kufanyika katika ajira mpya za taaluma hiyo.
"Wakati wa kutangaza nafasi mpya za ualimu, wakitaka kupata kazi, watafanya mtihani haijalishi tayari umesoma, kwanza itatuondolea matatizo. Na kuajiriwa kuwa Mwalimu utafanya mtihani, utaona matokeo, tutaangalia idadi inayohitajika tutachukua waliofaulu tutawaajiri," Amesema Prof.Mkenda.
Aidha Prof. Mkenda amebainisha maandalizi ya muongozo wa kuchukua walimu wa kujitolea, huku akidokeza tafakari inafanyika kuona uwezekano wa kuanzisha mafunzo tarajali kwa walimu.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amesema Shindano lilifanyika kwa njia ya kushindanisha video zenye umahiri katika maeneo yaliyotajwa. Video shindani zilipaswa kuwa na sifa kadhaa ambazo ni urefu usiozidi dakika kumi na tano, maudhui yaendana na umahiri uliokusudiwa na umri wa wanafunzi, ufundishaji unaowafanya wanafunzi kuwa kitovu cha ujifunzaji, mwalimu kuonesha umahiri wa matumizi ya teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji.
"Sifa nyingine zilikuwa ni mwalimu kuwasilisha somo kwa kueleweka, kufuata mtiririko mzuri na kuonesha mawasiliano mazuri kati yake na wanafunzi, mwalimu kuonesha ubunifu katika matumizi ya mbinu za ufundishaji ili kuwavutia wanafunzi na kufanya somo livutie na kueleweka kwa urahisi". Amesema
Pamoja na hayo amesema kuwa Shindano hilo, lilianza mwezi Aprili mwaka huu na video za walimu kutoka halmashauri 26 zilikusanywa zikiwa na maudhui ya kufundisha Hesabu na kuhesabu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akizungumza katika hafla ya Utoaji Tuzo kwa walimu walioshinda shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati, lililoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambayo imefanyika jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa akizungumza katika hafla ya Utoaji Tuzo kwa walimu walioshinda shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati, lililoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambayo imefanyika jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla ya Utoaji Tuzo kwa walimu walioshinda shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati, lililoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambayo imefanyika jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda wakipata picha ya pamoja na Washindi wa shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika Jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda wakipata picha ya pamoja na Washindi na majaji wa shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika Jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam
Wadau pamoja na walimu wakiwa katika hafla ya Utoaji Tuzo kwa walimu walioshinda shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati, lililoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambayo imefanyika jana Juni 16,2023 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Social Plugin