Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu,akizungumza wakati akifungua Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Makundi Maalum,Bw.Juma Samwel ,akielezea lengo la warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa uratibu na uendelezaji wa Utafiti,Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) Dkt Bugwesa Zabron Katale, akizungumza wakati wa Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,akizungumza wakati wa Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya Washiriki wakiwa katika warsha ya iliyoratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum iliyofanyika leo Juni 22,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIBU Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jmii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. John Jingu,amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kisayansi kufanya tafiti mbalimbali zitazotoa majibu ya kuongeza uzalishaji na vipato vya watu walio katika makundi maalum nchini.
Dk.Jingu ameyasema hayo leo Juni 22,2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya utengenezaji wa Vijarida sera vitakavyotatua changamoto za Makundi Maalum.
Dk. Jingu amesema kuwa sayansi na teknolojia inaweza kutumika katika kusaidia kupata majawabu yenye ushahidi ili kusaidia makundi maalum.
“Ni matarajio yetu kikao kazi hiki ni makubwa kwani tunatarajia majawabu yenye ushahidi na yanatokelezeka ili kupata njia nzuri zaidi za kusaidia Makundi Maalum katika kuinua hali yao ya kiuchumi”Alisema Dk. Jingu.
Amesema Mazingira yanaruhusu kuja na majawabu yenye ushahidi kwani miundombinu ipo na imesambaa nchini ikiwemo barabara, nishati, taasisi binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Mkurugenzi wa idara ya Makundi Maalum kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Juma Samwel amesema serikali inapambana kuhakikisha wafanyabiashara ndogondogo wanakua kiuchumi.
“Tunatamani Makundi haya maalum yaweze kurahisishiwa mazingira ya kufanyia kazi kwa kushirikishwa kwa ukaribu katika masuala yanayowahusu lakini pia mamlaka husika na yanayowagusa wazalishaji hawa wadogo kufanya nao kazi kwa ukaribu ili kurahisisha uzalishaji wao kwa mfano Latra kuweza kuongeza ukaribu nao ikiwemo kuwaelemisha juu ya masuala mbalimbali”
Aidha, Mkurugenzi wa uratibu na uendelezaji wa Utafiti, Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) Dk. Bugwesa Zabron Katale amesema lengo kubwa la taasisi ni kutatua changamoto zinazokumba Jamii katika kada mbalimbali.
“Lengo kubwa la Tume ya Sayansi na Utafiti ni kutatua changamoto zinazoikumba jamii kupitia tafiti mbalimbali na kuja na masuluhisho yatauowezesha kuleta mabadiliko na maendeleo katika Taifa.Hivyo kuwa na Taifa linalofanya vitu kitaalam na si kwa mazoea”
Social Plugin