Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Kongwa Dk. Omari Nkulo akifungua mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwenye mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake katika kata ya Mtanana wilayani Kongwa mapema jana.
*********************
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wilaya ya Kongwa Dk. Omari Nkulo amewataka washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwenye mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake katika kata ya Mtanana wilayani Kongwa kuzingatia mafunzo hayo ili kuweza kulinda afya za walaji na uchumi kwa ujumla.
“Nawasihi sana kuzingatia mafunzo haya kwani tukielewa na kutekeleza itatusaidia kulinda afya za walaji na hata kufaidika kiuchumi kwani mahindi yetu na nafaka zingine zitakua salama kuuza katika soko la ndani na nje ya nchi “alisema Dk.Nkulo
Vilevile Dk.Nkulo alishukuru Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa mafunzo hayo na kutoa wito kwa washiriki kuwa mabalozi wa sumukuvu kwa wengine.
Dk.Nkulo ametoa wito huo kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la viwango Tanzania (TBS)kupitia mradi wa kudhibiti sumukuvu Tanzania (TANIPAC).
Mafunzo hayo yanayoendelea wilayani Kongwa yameshafanyika wilayani Kiteto na yanategemewa kufanyika katika wilaya ya Gairo na Kilosa.
Social Plugin