SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika maaadhimisho ya Wiki ya Barcode Kitaifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo Shirika limeendela kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za zenye ubora na zinazokidhi matakwa ya Viwango.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Bi. Beatrice Lema amesema ili kuwa wazalishaji wanatakiwa kuzalisha bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango kwani kwa kufanya hivyo taifa litapata nguvu kazi kubwa kwani walaji na watumiaji wa bodhaa hizi hawataathirika na bidhaa hafifu.
Aidha ameongeza kuwa TBS kushiriki katika maadhimisho haya ni fursa kwa wajasirimali kwani wanatembelewa katika mabanda yao na kuelezwa taratibu za kupata alama ya ubora ili wazalishe bidhaa bora na salama kwa kuxingatia matakwa ya viwango wakiwa katika mabanda yao pasipo kupata usumbufu.
"TBS imetumia maonesho haya kama sehemu ya kutoa elimu kwa wajasiriamali kwa kuwatembelea katika mabanda yao na kuwaeleza jinsi wanavyoweza kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bila gharama yoyote suala amabalo litawasaidia kupata masoko ndani na nje ya nchi na pia kuwa na ushindani sawia kwa bidhaa zinazopatikana sokoni.
Kwa upande wake Afisa Masoko (TBS) Bi. Rhoda Mayugu amesema, Shirika limepata nafasi ya kutoa elimu kwa watumiaji wa bidhaa likiwahimiza kuhusu umuhimu wa kusoma taarifa katika bidhaa ili kuwa na utamaduni wa kujiepusha na bidhaa hafifu.
“TBS imetumia maoesho haya kama eneo la kutoa elimu kwa watumiaji wa bidhaa kwani hawa ndio waathirika wakubwa wa bidhaa hafifu, tumewasisitiza kuhakikisha wanasoma maelezo ya bidhaa husika hususani muda wa matumizi wa bidhaa husika pamoja na nembo ya ubora ili kujihakikishia kuwa bidhaa wanazotumia ni bora na salama.
Social Plugin